Afisa Biashara Arusha apongeza ukuwaji wa Biashara wa Jiji la Dodoma

Na. Mwandishi wetu, DAR ES SALAAM

 

HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imepongezwa kwa kasi ya ukuaji wa shughuli za biashara na uwekezaji na kutajwa kuwa ni fursa kwa watanzania na wageni kuwekeza.

 


Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji Halmashauri ya Jiji la Arusha, John Kilunge alipotembelea banda la Halmashauri ya Jiji la Dodoma katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

Kilunge alipongeza kasi ya ukuaji wa shughuli za biashara na uwekezaji ndani ya jiji hilo na kusema kuwa ni fursa kwa watanzania na wageni kuwekeza na kufungua zaidi fursa za ajira.

Akiwa katika banda hilo, alipata maelezo kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na Halmashauri ya Jiji la Dodoma pamoja na fursa za uwekezaji zilizopo, hususan katika sekta za ardhi, biashara na maendeleo ya kiuchumi.

Alisema kuwa Jiji la Dodoma linaonesha mafanikio makubwa katika kukuza mazingira ya biashara na kuvutia wawekezaji kupitia mipango yake ya maendeleo na upanuzi wa huduma kwa wananchi. “Dodoma inaonesha mwelekeo mzuri wa ukuaji wa biashara na uwekezaji. Ni jiji linalokua kwa kasi na lenye fursa nyingi kwa wafanyabiashara na wawekezaji” alisema Kilunge.

 


Akiwa katika banda hilo Afisa Biashara wa Jiji la Dodoma, Ruth Kingu alimueleza kuwa  maonesho hayo yamekuwa jukwaa muhimu la kuutangaza uwezo wa Jiji la Dodoma katika biashara, uwekezaji na utoaji wa huduma. Alisema kuwa maonesho hayo yanasaidia kujenga ushirikiano na wadau kutoka maeneo mbalimbali nchini.

Kwa upande wake, mkazi wa Kahama aliyetembelea banda hilo, Kisumu Nyamtela alisema kuwa ushiriki wa jiji hilo katika Maonesho ya Sabasaba unalenga kutangaza huduma zinazotolewa na halmashauri pamoja na fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo. “Ninawiwa kutembelea Dodoma kujionea kulivyobadilika, mnajitangqza vizuri sana” alisema Nyamtela.

Comments

Popular Posts

Jiji la Dodoma lashauriwa kulinda hadhi ya Makao Makuu ya Nchi

Jiji la Dodoma latangaza fursa za Uwekezaji katika Maonesho ya Sabasaba, 2026