RC Senyamule aridhishwa maendeleo ya ujenzi Jengo Jumuishi Kituo cha Afya Makole

Na. Mwandishi wetu, DODOMA

HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imepongezwa kwa usimamizi mzuri wa ujenzi wa mradi wa jengo jumuishi la Kituo cha Afya Makole ukitajwa baada ya kukamilika kuwa utaboresha utoaji wa huduma za afya kwa wananchi.



Pongezi hizo zilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule alipofanya ziara ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo jana.

Mkuu wa mkoa alisema kuwa kukamilika mradi huo kutaleta mapinduzi makubwa katika utoaji wa huduma za afya katika halmashauri. Alisema kuwa jengo hilo linajengwa eneo la kimkakati katikati ya jiji likizungukwa na taasisi za serikali na binafsi.

“Jengo hili litapanua huduma ambazo hazikuwepo hapo awali, ikiwemo huduma za dharura, huduma za uzazi na huduma nyingine za kibingwa. Huu ni mradi muhimu ambao utawawanufaisha wananchi wengi. Niwapongeze sana Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa usimamizi mzuri,” alisema Senyamule.

Alitumia wakati huo kuwapongeza watumishi wa Kituo cha Afya Makole kwa kuendelea kutoa huduma bora zinazowavutia wananchi licha ya uwepo wa hospitali nyingine nyingi jijini Dodoma.

“Idadi kubwa ya wananchi, hususan wajawazito, wanaendelea kufika hapa kupata huduma kwa sababu huduma zinazotolewa ni bora. Huduma bora ndiyo zinazojenga imani ya wananchi na kuongeza idadi ya wanaofika kupata matibabu,” alisisitiza.

Comments

Popular Posts

Jiji la Dodoma lashauriwa kulinda hadhi ya Makao Makuu ya Nchi

Afisa Biashara Arusha apongeza ukuwaji wa Biashara wa Jiji la Dodoma

Wakili Kipangula asisitiza weledi taaluma ya habari