Jiji la Dodoma latakiwa kushirikisha wadau afua za Lishe

Na. Mwandishi Wetu, DODOMA

HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imetakiwa kuongeza ushirikishaji wa makundi mbalimbali ya jamii katika kuimarisha afua za lishe ili kuhakikisha elimu na huduma za lishe bora zinawafikia wananchi wote.



Wito huo ulitolewa na Mwenyekiti wa Kikao cha Tathmini ya Mkataba wa Lishe kwa Robo ya Nne Aprili-Juni, 2026 Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Sakina Mbugi alipoongoza kikao hicho kwa niaba ya mkuu wa wilaya kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri.

Mbugi ambae ni katibu tawala wilaya ya Dodoma alisema kuwa ni muhimu kuwashirikisha vijana waliopo nje ya mfumo rasmi, wazee, viongozi wa dini, viongozi wa mila, taasisi za serikali na binafsi, watu mashuhuri pamoja na kaya katika kuhamasisha na kutoa elimu ya lishe bora.

Alisema kuwa ushirikishwaji wa makundi mbalimbali ya jamii ni muhimu katika kuongeza uelewa na kuleta matokeo chanya na kubainisha kuwa lishe bora haihusu watoto pekee bali watu wa rika zote.






“Sisi, timu ya wataalam, tupo tayari kuhakikisha kuwa makao makuu ya nchi yanazingatia lishe bora. Jitihada za kuhimiza lishe bora zinaanza na mimi binafsi, kisha zinakufikia wewe na hatimaye jamii kwa ujumla,” alisema Mbugi.

Naye, Kaimu Afisa Lishe wa Jiji la Dodoma, Happiness Mlamka alisema kuwa utekelezaji wa viashiria vya lishe kwa kipindi cha Mwezi Aprili hadi Juni, 2026 umeonesha mafanikio makubwa. Alisema kuwa huduma muhimu za lishe zikiwemo utoaji wa virutubisho na matibabu kwa watoto wenye utapiamlo zimefikia malengo yaliyowekwa.

Comments

Popular Posts

Jiji la Dodoma lashauriwa kulinda hadhi ya Makao Makuu ya Nchi

Afisa Biashara Arusha apongeza ukuwaji wa Biashara wa Jiji la Dodoma

Wakili Kipangula asisitiza weledi taaluma ya habari