Jiji la Dodoma lajinoa kuelekea SHIMISEMITA 2026
Na. Mwandishi Wetu, DODOMA
Timu
ya Mpira wa Pete ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma inaendelea kujinoa kuelekea
mashindano ya SHIMISEMITA 2026 yanayotarajiwa kufanyika Mwezi Agosti, 2026 jijini
Mbeya, mara baada ya kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Timu ya Jamhuri kabla
ya kuingia kwenye dimba la mashindano rasmi.
Hayo aliyasema Afisa Michezo wa Jiji la Dodoma, Neema kilongola mara baada ya kutamatika kwa mchezo huo katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma
Alisema kuwa michezo ya kirafiki ni sehemu muhimu ya maandalizi kwa kuwa husaidia kubaini mapungufu na kuyafanyia kazi mapungufu hayo. "Lengo la mchezo huu wa kirafiki halikuwa kushinda pekee, bali ilikuwa ni kujipima uwezo wetu, kubaini mapungufu yaliyopo na kuyafanyia kazi kabla ya kuanza mashindano ya SHIMISEMITA. Tunaendelea kujenga timu imara na tunaamini tutafika Mbeya tukiwa katika kiwango kizuri cha ushindani " alisema Kilongola.
Aliongeza
kuwa kikosi hicho kinaendelea na programu maalum za mazoezi zinazolenga
kuimarisha mbinu za uchezaji, kasi, mawasiliano ya ndani ya uwanja pamoja na
utimamu wa mwili ili kuhakikisha kinakuwa tayari kwa ushindani mkubwa
unaotarajiwa katika mashindano hayo yanayokutanisha halmashauri mbalimbali
nchini.
Katika mchezo huo, timu ya Jamhuri iliibuka na ushindi wa mabao 37 kwa 7, matokeo ambayo yameipa timu ya Jiji nafasi ya kutathmini kiwango chake na kuendelea kuboresha maandalizi kabla ya mashindano. Licha ya kupoteza mchezo huo, wachezaji wa Jiji la Dodoma wameendelea kuonyesha ari na kujiamini, wakiahidi kupambana kwa nguvu zote na kuibuka kidedea katika mashindano ya SHIMISEMITA 2026 mkoani Mbeya.
Comments
Post a Comment