Posts

Kata ya Ng’hong’onha mwenyeji Siku 16 za Kupinga Ukatili

Image
Na. Mwandishi wetu, Ng’hong’onha Kata ya Ng’hong’onha mwenyeji wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ngazi ya halmashauri yakilenga kutoa elimu na hamasa kwa jamii dhidi ya kupambana na ukatili katika jamii kuelekea miaka 30 ya Beijing. Katika maadhimisho hayo elimu dhidi ya ukatili wa kijinsia itatolewa pamoja na kufafanua aina za ukatili wa kijinsia, taarifa za vitendo vya ukatili wa kijinsia na kuwajengea uelewa wanafunzi na watoto kuripoti taarifa za ukatili wa kijinsia katika jamii. Maeneo mengine yatakayopewa kipaumbele ni umuhimu wa kuwainua wanawake kiuchumi kama njia moja wapo ya kupambana na ukatili wa kijinsia. Maadhimisho hayo yanayoongozwa na kaulimbiu isemayo “Kuelekea miaka 30 ya Beijing: Chagua kutokomeza ukatili wa kijinsia” yanapambwa na burudani mbalimbali kama maigizo na ngoma, mgeni rasmi ni Joseph Chotero, Mkurugenzi wa SABUDA Foundation yakifanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi Ng’hong’onha. MWISHO

Rais, Dkt. Samia aagiza fedha za maadhimisho ya Uhuru kutumika kwenye huduma za kijamii- Majaliwa

Image
  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameelekeza   Maadhimisho ya Miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara kwa Mwaka 2024 yafanyike katika ngazi ya mikoa na Fedha zilizotengwa katika kila taasisi kwa ajili ya Maadhimisho hayo zielekezwe katika kutoa huduma za kijamii. Amesema kuwa kila mkoa uhakikishe Wilaya zake zinafanya shughuli za kijamii ikiwemo upandaji miti, usafi wa mazingira katika maeneo ya kijamii kama vile kwenye Masoko, Hospitali, Kambi za wazee na wenye mahitaji maalum, mashindano ya michezo mbalimbali pamoja na makongamano na midahalo ya kujadili maendeleo endelevu ambayo nchi yetu imefikia katika kipindi cha miaka 63 ya Uhuru.  Amesema hayo leo Jumatano (Desemba 04, 2024) katika kikao kazi cha Mawaziri kilichofanyika katika ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma. “Sherehe za Mwaka huu hazitakuwa na Gwaride na Shughuli nyingine za Kitaifa ” . Amesema kuwa Serikali inatoa wito kwa Wananchi kushiriki katika shughuli hiz...

Jiji la Dodoma washiriki maadhimisho ya Siku ya Ukimwi ngazi ya mkoa

Image
  Baadhi ya wataalam wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma muda mfupi kabla ya kuanza mwendo kuelekea Halmashauri ya Wilaya ya Chemba kushiriki maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani yanayofanyika ngazi ya mkoa. Kaulimbiu ni " CHAGUA NJIA SAHIHI, TOKOMEZA UKIMWI "

Mtaa kinara upigaji kura

Siku ya Uchaguzi

Mtaa wa Mnyakongo Kata ya Nkuhungu wajitokeza kupiga kura Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Image
 

Mtaa wa Chang'ombe mstari wa mbele kupiga kura Kata ya Ihumwa

Image
 

Diwani Miyuji aongoza wakazi wa Mtaa wa Mwatano kupiga kura

Image
 

Wakazi wa Chang'ombe, Kata ya Ihumwa wajitokeza kupiga kura

Image
Wakazi wa Mtaa wa Chang'ombe, Kata ya Ihumwa wajitokeza mapema kupiga kura Uchaguzi wa Serikali za Mitaa leo katika Kituo cha Shule ya Msingi Msuguri

Matukio katika Picha Semina ya Wasimamizi wa Vituo vya kupigia kura katika Ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la DOdoma uliopo Mji wa Serikali Mtumba

Image
Mhe. TheresianKiwango, Hakimu Mkazi