Kata ya Ng’hong’onha mwenyeji Siku 16 za Kupinga Ukatili
Na. Mwandishi wetu, Ng’hong’onha
Kata ya Ng’hong’onha mwenyeji wa maadhimisho ya siku
16 za kupinga ukatili wa kijinsia ngazi ya halmashauri yakilenga kutoa elimu na
hamasa kwa jamii dhidi ya kupambana na ukatili katika jamii kuelekea miaka 30
ya Beijing.
Katika maadhimisho hayo elimu dhidi ya ukatili wa
kijinsia itatolewa pamoja na kufafanua aina za ukatili wa kijinsia, taarifa za
vitendo vya ukatili wa kijinsia na kuwajengea uelewa wanafunzi na watoto kuripoti
taarifa za ukatili wa kijinsia katika jamii. Maeneo mengine yatakayopewa
kipaumbele ni umuhimu wa kuwainua wanawake kiuchumi kama njia moja wapo ya
kupambana na ukatili wa kijinsia.
Maadhimisho hayo yanayoongozwa na kaulimbiu isemayo “Kuelekea
miaka 30 ya Beijing: Chagua kutokomeza ukatili wa kijinsia” yanapambwa na
burudani mbalimbali kama maigizo na ngoma, mgeni rasmi ni Joseph Chotero,
Mkurugenzi wa SABUDA Foundation yakifanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi Ng’hong’onha.
MWISHO
Comments
Post a Comment