KATA YA CHAMWINO YATOA ELIMU YA UKATILI WA KIJINSIA
Na. Dennis Gondwe, CHAMWINO
Timu
ya wataalam kutoka Kata ya Chamwino yajikita katika utoaji wa elimu ya kupinga
vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa makundi mbalimbali kwa lengo la kuhakikisha
uelewa mpana katika mapambano hayo unaenea kwa jamii.
Akielezea maeneo yaliyopewa kipaumbele na timu hiyo katika kutoa elimu, Afisa Mtendaji kata ya Chamwino, Lucas Nkelege alisema kipaumbele ni kutoa elimu kwa jamii.
Alisema
kuwa timu hiyo ilijikita katika kuelezea wajibu wa wazazi na walezi katika
makuzi ya watoto na sheria inayomlinda mtoto Namba 21 ya mwaka 2009. Maeneo
mengine yaliyopewa msisitizo ni umuhimu wa ulinzi wa watoto wa kiume na madhara
kwa watoto hao endapo hawatapewa uangalizi wa karibu na hatua za kufanya pale
mtoto amapofanyiwa ukatili.
Aidha,
wazazi na walezi walitaarifiwa uwepo wa kituo cha huduma za pamoja na msaada
kwa watoto waliofanyiwa ukatili (one stop center).
Nkelege
alisema kuwa timu shirikishi ya wataalamu ya Kata ya Chamwino iliongozwa na Afisa
Mtendaji kata ya Chamwino, ikiwa na Afisa ushirikishwaji wa Jeshi la Polisi wa
Kata ya Chamwino, Afisa Ustawi wa Jamii, Afisa Maendeleo ya Jamii walishiriki
kutoa elimu ya kupinga ukatili wa kijinsia kwenye misitiki, na vijiwe vya
bodaboda katika Kata ya Chamwino.
MWISHO
Comments
Post a Comment