Agenda ya Lishe yaongeza Ari ya usomaji S/M Dodoma Makulu
Na. Abdul Iddi, DODOMA MAKULU
Shule ya Msingi Dodoma Makulu imeshukuru agenda ya Rais,
Dkt. Samia Suluhu Hassan ya lishe shuleni kwa sababu inawaongezea ari ya kusoma
na kupata matokeo yanayokusudiwa.
Shukrani hiyo ilitolewa na Mwalimu wa Lishe, Rehema Kalinga alipokuwa akiongea na waandishi wa Habari waliotembelea shule ya msingi Dodoma makulu kujionea hali ya lishe kwa wanafunzi shuleni hapo.
Alisema kuwa shule yake inazingatia ajenda ya Lishe kwa
kuwapa wanafunzi wote kuanzi awali mpaka darasa la Saba uji. Darasa la Nne na
la Saba kupata chakula cha mchana. “Toka ajenda hii kuanza kutekelezwa,
tumeanza kuona matokeo Chanya. Kwanza kwakupunguza utoro, pia watoto darasani
wanafundishika” alisema Mwl. Kalinga.
Aidha, alitoa pongezi kwa wazazi kwa kusikiliza ajenda
ya Lishe na kuitekeleza bila kusuasua kwasababu waliweza kutoa mchango kwa
kiasi walicho kubaliana na kamati ya wazazi wa shule hiyo. “Muitikio ni mkubwa
kwasababu watoto wote katika Shule ya Dodoma Makulu wanapata uji na wengine pia
chakula cha mchana, kwasababu wazazi hawakukaa nyuma kutoa mchango kwaajili ya
watoto wao kupata chakula shuleni” alisema Kalinga.
Nae Mwalimu wa Taaluma wa shule hiyo, Mwl. Mwanahamisi
Goma alieleza namna serikali ya awamu ya sita inavyotoa kipaumbele kwa agenda
ya lishe na kusema kuwa inasaidi kukuza taaluma. “Suala la lishe limenisaidia
sana katika utendaji kazi wangu wa uratibu wa taaluma hapa shuleni, kwasababu
kupitia chakula shuleni wanafunzi wa shule wameonekana kuongeza ufahulu kwa
kiasi kikubwa ukilinganisha na wakati ambao walikuwa hawapati chakula. Ufaulu wetu
umepanda kuanzia ngazi ya kata mpaka kitaifa” alisema Mwl. Goma.
Nae mwanafunzi wa darasa la Sita, Jonathan Mwasambuli alieleza
jinsi agenda ya lishe ilivyowasaidia katika masomo. “Chakula shuleni kinasaidia
kupata nguvu pia kuimarika kiubongo pia inanifanya nishindwe kulala darasani. Hivyo,
chakula kinanipa nguvu ya kusoma kwa bidi” alisema Mwasambuli.
MWISHO
Comments
Post a Comment