Afisa Tabibu Zahanati ya Zuzu atoa elimu ya Lishe kwa vitendo

Na. Ramadhani Mohammed, ZUZU

Afisa Tabibu wa Zahanati ya Zuzu jijini Dodoma ametoa elimu ya lishe kwa wazazi na walezi kwa njia ya vitendo, akisisitiza umuhimu wa kuhakikisha watoto wanapata chakula bora na chenye virutubisho muhimu kwa ukuaji na afya zao.



Akitoa elimu hiyo, Afisa Tabibu huyo aliwaonesha wazazi na walezi namna ya kuchagua na kuchanganya vyakula mbalimbali vinavyopatikana katika mazingira yao ili kupata mlo kamili unaokidhi mahitaji ya mtoto.

Alisema kuwa lishe bora inaanzia katika familia, hivyo wazazi na walezi wanapaswa kuwa na uelewa sahihi kuhusu aina ya vyakula, namna ya kuviandaa pamoja na kiasi kinachofaa kwa watoto kulingana na mahitaji yao.

Aidha, alisisitiza umuhimu wa kuzingatia usafi wakati wa kuandaa, kupika na kuhifadhi chakula, akieleza kuwa lishe bora ikiambatana na usafi husaidia kulinda afya ya mtoto na kupunguza hatari ya magonjwa.


Alisema kuwa elimu hiyo imetolewa kwa vitendo ili kuwapa wazazi uelewa unaoweza kutumika moja kwa moja katika maisha ya kila siku, hususan katika kutumia vyakula vinavyopatikana kwa urahisi katika maeneo yao.

Aliwataka wazazi na walezi kuendelea kuzingatia elimu wanayopewa na wataalamu wa afya, pamoja na kuhakikisha watoto wanapata mlo bora na unaozingatia mahitaji yao ya kiafya.

Comments

Popular Posts

Mvua za El Nino: DC Shekimweri awaasa wananchi wa Dodoma Kuchukua Tahadhari

Jiji la Dodoma Biashara saa 24, usafi saa 24

Wananchi Dodoma wahimizwa kufanya usafi wa Mazingira kila siku