Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj. Jabir Shekimweri, akiongozana na Kamati ya Maafa ya Wilaya ya Dodoma, ametembelea na kukagua maeneo mbalimbali katika Kata ya Mkonze yanayodhaniwa kuwa katika hatari ya kuathiriwa na mvua kubwa, ikiwa ni sehemu ya hatua za Serikali za kujiandaa na kukabiliana na athari za mvua za El Niño
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj. Jabir Shekimweri,
akiongozana na Kamati ya Maafa ya Wilaya ya Dodoma, ametembelea na kukagua
maeneo mbalimbali katika Kata ya Mkonze yanayodhaniwa kuwa katika hatari ya kuathiriwa
na mvua kubwa, ikiwa ni sehemu ya hatua za Serikali za kujiandaa na kukabiliana
na athari za mvua za El Niño
Ziara hiyo imelenga kubaini maeneo yenye changamoto, ikiwemo mifereji ya maji na maeneo mengine yanayoweza kuhatarisha usalama wa wananchi, ili hatua stahiki za maboresho na tahadhari zichukuliwe mapema.
Hatua hiyo ni muendelezo wa jitihada za Serikali
katika kuhakikisha maeneo hatarishi yanatambuliwa na kufanyiwa maboresho kwa
wakati, sambamba na kuwaelimisha wananchi kuchukua tahadhari na kuzingatia
maelekezo ya mamlaka ya hali ya hewa.
Katika ziara hiyo, Kamati ya Maafa imeendelea kutoa
msisitizo juu ya umuhimu wa ushirikiano kati ya Serikali na wananchi katika
kuzuia athari zinazoweza kusababishwa na mvua kubwa, hususani katika maeneo
yenye miundombinu ya kupitisha maji.



Comments
Post a Comment