Jiji la Dodoma latenga Bil. 3.9 kuongeza miundombinu mapokezi ya Kidato cha Kwanza 2027
Na. Dennis Gondwe, KIKUYU KUSINI
HALMASHAURI
ya Jiji la Dodoma imetenga shilingi 3,956,990,000 katika Bajeti ya Mwaka wa Fedha
2026/2027 kwa ajili ya kuongeza miundimbinu ya madarasa, viti, meza na matundu
ya vyoo ikiwa ni maandalizi ya kupokea wanafunzi watakaohitimu darasa la sita
na saba kwa pamoja.
Kauli
hiyo ilitolewa na Kaimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Wella, Mwl. Allen Lugemalila
wakati akisoma
taarifa ya mradi wa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika Shule ya Sekondari
Wella kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Mwaka 2026, shuleni hapo.
“Ndugu
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026, halmashauri inategemea kupokea
wanafunzi watakaohitimu darasa la sita na la saba kwa pamoja mwaka 2027. Katika
kufanikisha mpango huo wa serikali, kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027, halmashauri
imetenga bajeti ya shilingi 3,956,990,000 kwa lengo la kuongeza miundombinu ya
madarasa, vyoo, viti na meza. Pamoja na lengo hili la msingi, shule hii ilikuwa
na uhitaji wa vyumba viwili vya madarasa ili kuweza kukidhi ongezeko la ufaulu
kwa wanafunzi waliohitimu darasa la saba 2025” alisema Mwl. Lugemalila.
Kiongozi
wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Wazo Mwang’onda aliipongeza serikali kwa
kuendelea kuboresha miundombinu ya elimu na kuwawezesha wanafunzi kusoma katika
mazingira mazuri.
Shule ya Sekondari Wella ilisajiliwa
tarehe 06 Januari, 2008 ikiwa na jumla ya wanafunzi 915 na walimu 66 ikiendelea kuiishi kaulimbiu ya Mwenge wa Uhuru
isemayo ‘Tanzania ni yetu sote, tushikamane kwa pamoja kuleta maendeleo’.
Comments
Post a Comment