Wilaya ya Dodoma yapata “clean sheet” Miradi ya Mwenge wa Uhuru 2026

Na. Dennis Gondwe, DODOMA

Jumla ya miradi saba ya maendeleo yenye thamani ya shilingi Bil. 9,823,862,925 iliyotembelewa na Mwenge wa Uhuru Mwaka 2026 katika Wilaya ya Dodoma imepitishwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Mwaka 2026 ili iweze kutoa huduma kwa wananchi.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2026 (kulia) akizindua mradi wa madarasa mawili katika Shule ya Sekondari Wella

Miradi iliyozinduliwa na Mwenge wa Uhuru Mwaka 2026 ni mradi wa Nishati safi ya kupikia katika Shule ya Sekondari Dr. Samia-Dodoma wenye thamani ya shilingi 698,800,161, mradi wa uwekezaji binafsi wa Hoteli ya Starline wenye thamani ya shilingi 3,000,000,000 ukiwa pamoja na kutembelea mradi wa kusimika kamera za usalama wenye gharama ya shilingi 682,561,548, mradi wa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa Shule ya Sekondari Wella wenye thamani ya shilingi 42,800,000, mradi wa Maji safi Kata ya Nala unaotekelezwa na Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira na ujenzi wa Barabara kwa kiwango cha lami yenye urefu wa Kilimeta 1.6 kutoka Barabara iendayo Singida hadi Hospitali ya Jiji wenye thamani ya shilingi 2,872,857,693.

Mradi mmoja wa ujenzi wa majengo matatu (upasuaji, wodi ya wanaume na kufulia) katika Hospitali ya Jiji wenye thamani ya shilingi 800,000,000 uliwekewa jiwe la msingi.

Mwenge wa Uhuru Mwaka 2026 unaongozwa na kaulimbiu isemayo ‘Tanzania ni Yetu Sote, Tushikamane Kwa pamoja Kuleta Maendeleo’ katika wilaya ya Dodoma ulikimbia umbali wa kilomita 86.3.


Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026 akizindua Mradi wa Maji Kata ya Nala


Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026 (watatu kulia) akizindua mradi wa Barabara ya Kilimeta 1.6 kiwango cha lami
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026 akizindua Hoteli ya Starline 

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026 (kulia) akizindua mradi wa Nishati safi ya kupikia katika Shule ya Sekondari Wella



MWISHO

Comments

Popular Posts

Jiji la Dodoma lashauriwa kulinda hadhi ya Makao Makuu ya Nchi

Afisa Biashara Arusha apongeza ukuwaji wa Biashara wa Jiji la Dodoma

Jiji la Dodoma latenga Bil. 3.9 kuongeza miundombinu mapokezi ya Kidato cha Kwanza 2027