Ukarabati Soko Kuu Majengo wafikia 80%

Ukarabati wa Soko la Majengo umefikia asilimia 80 ya utekelezaji, hatua inayoashiria kuwa mradi huo unakaribia kukamilika na kuanza kutoa huduma zilizokusudiwa kwa wananchi na wafanyabiashara.


Mradi huo wenye thamani ya shilingi bilioni 4.8 unalenga kuboresha mazingira ya soko, kuimarisha miundombinu na kuongeza ufanisi wa shughuli za biashara kwa wafanyabiashara na wananchi.


Ukarabati huo unatarajiwa kuongeza usalama, usafi na mvuto wa soko, sambamba na kutoa mazingira bora zaidi ya biashara na kuchochea shughuli za kiuchumi katika eneo hilo.




Comments

Popular Posts

Polisi Kata waungana zoezi la Usafi wa Mazingira Dodoma

DC Shekimweri afanya ukaguzi wa usafi Kata ya Kizota

Dodoma kuanza awamu ya pili ya Kampeni ya Chanjo ya Polio tarehe 29 Septemba, 2026