Dodoma kuanza awamu ya pili ya Kampeni ya Chanjo ya Polio tarehe 29 Septemba, 2026

Na. Mwandishi wetu, DODOMA

 

Wazazi na walezi katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma wametakiwa kuhakikisha watoto wanapata chanjo ya Polio katika awamu ya pili ya kampeni hiyo, inayotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 29 Septemba hadi tarehe 2 Oktoba, 2026.

 


Akizungumza katika kipindi cha Amka Tofauti kinachorushwa na Kituo cha Redio A FM, Afisa Tabibu wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dkt. Ngoyeji Nkinga, alisema kuwa ushiriki wa wazazi na walezi ni muhimu katika kuhakikisha watoto wote wanaolengwa wanapata chanjo hiyo.

 

“Wazazi na walezi wahakikishe watoto walio chini ya miaka 10 wanapata chanjo ya Polio kwasababu chanjo hii ni salama na muhimu kwa watoto ili kuwalinda dhidi ya ugonjwa polio,” alisema Dkt. Nkinga.

 

Alisema kuwa chanjo ya Polio ina umuhimu mkubwa katika kuzuia madhara yanayoweza kusababishwa na ugonjwa huo, hivyo jamii inapaswa kuchukua hatua kuhakikisha watoto wanapatiwa chanjo kwa wakati.

 

Aidha, aliwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa wahudumu wa afya watakaoshiriki katika kampeni hiyo, pamoja na kufuatilia taarifa rasmi kuhusu maeneo na utaratibu wa utoaji wa chanjo.

 

Kampeni hiyo ya awamu ya pili itaanza tarehe 29 Septemba na kumalizika tarehe 2 Oktoba 2026, huku wazazi na walezi wakihimizwa kushiriki kikamilifu katika kuhakikisha watoto wanaolengwa wanapata chanjo.

Comments

Popular Posts

Jiji la Dodoma Biashara saa 24, usafi saa 24

Mvua za El Nino: DC Shekimweri awaasa wananchi wa Dodoma Kuchukua Tahadhari

Wananchi Dodoma wahimizwa kufanya usafi wa Mazingira kila siku