DC Shekimweri afanya ukaguzi wa usafi Kata ya Kizota
Na. Mwandishi wetu, KIZOTA
Mkuu
wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri, amefanya ukaguzi wa hali ya usafi
katika maeneo mbalimbali ya biashara yaliyopo Kata ya Kizota, ikiwa ni sehemu
ya kampeni ya kuhamasisha usafi wa mazingira katika Halmashauri ya Jiji la
Dodoma.
Katika ukaguzi huo, amefuatilia hali ya usafi wa maeneo ya biashara pamoja na mazingira yanayozunguka, huku akihimiza wafanyabiashara na wananchi kuhakikisha maeneo yao yanakuwa safi wakati wote.
Amesisitiza
kuwa usafi wa mazingira ni jukumu la kila mwananchi, hivyo wafanyabiashara
wanapaswa kushirikiana na serikali katika kuhakikisha maeneo yao ya biashara
yanakuwa safi, salama na yenye mazingira bora.
Ukaguzi
huo ni sehemu ya kuendeleza kampeni ya usafi wa mazingira katika Halmashauri ya
Jiji la Dodoma chini ya kaulimbiu isemayo “Dodoma Fahari Yetu, Usafi ni Wajibu
Wetu.”
Comments
Post a Comment