Dodoma Jiji yaifunga Mji Ifakara 41-3 Mpira wa Pete Mashindano ya SHIMISEMITA
Na. Mwandishi wetu, MBEYA
Timu ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma ya Mpira wa Pete Wanawake
imeishushia kipigo kizito Timu ya Halmashauri ya Mji Ifakara cha magoli 41-3 katika
siku ya pili ya Mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Serikali za Mitaa
Tanzania (SHIMISEMITA) yanayoendelea jijini Mbeya.
Mchezo huo ulianza kwa kasi katika dakika za mwanzo, lakini kadri muda ulivyokuwa ukiendelea Timu ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma ilionekana kuumiliki mchezo. Hadi kufikia tamati ya mchezo huo Timu ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma iliibuka na ushindi mnono wa magoli 41-3 ya Halmashauri ya Mji Ifakara.
Mchezo wa Mpira wa Mikono Wanaume Halmashauri ya Jiji la
Dodoma ililazimishwa sare ya 5-5 dhidi ya Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Aidha,
katika Mchezo wa Mpira wa Kikapu ya Wanaume Halmashauri ya Jiji la Dodoma
iliichakaza Timu ya Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha kwa vikapu 28-7.
Halmashauri ya Dodoma la Jiji iliendeleza kasi kwenye
mchezo wa Mpira wa Wavu kwa Wanaume, ikiichapa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduma
kwa seti 2-0. Seti ya kwanza ilimalizika kwa 25-1, kabla ya Dodoma Jiji
kushinda seti ya pili kwa 25-7.
Mchezo wa Mpira wa Mkono Wanawake, Halmashauri ya Jiji la
Dodoma ilitoshana nguvu na Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu kwa sare ya
0-0.
Comments
Post a Comment