Polisi Kata waungana zoezi la Usafi wa Mazingira Dodoma
Na. Mwandishi wetu, KIZOTA
Mapolisi Kata kutoka Kata za Kizota, Nkuhungu, Nala,
Chigongwe na Mbalawala wameungana na wananchi kushiriki katika zoezi la usafi
wa mazingira.
Akizungumza na waandishi wa habari, Inspector Baraka Nashoni amesema kuwa Jeshi la Polisi lipo tayari kushirikiana na wananchi katika shughuli za usafi na utunzaji wa mazingira, akieleza kuwa ushiriki wao unalenga kuhakikisha maeneo yanakuwa safi na salama.
Amehimiza wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la
Polisi katika shughuli mbalimbali za kijamii, ikiwemo usafi wa mazingira.
Comments
Post a Comment