Jiji la Dodoma lavuna Tuzo Tano Nanenane, 2026
Na. Mwandishi wetu, DODOMA
Halmashauri
ya Jiji la Dodoma imeibuka kidedea katika Maonesho ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
ya Nanenane Kitaifa 2026 baada ya kutwaa tuzo tano, hatua inayoonesha mafanikio
makubwa ya jiji hilo katika kuendeleza sekta za kilimo, mifugo na uvuvi.
Maonesho
hayo yaliyofanyika katika Viwanja vya Dkt. John Samuel Malecela jijini Dodoma
na kuhitimishwa Agosti 8, 2026 yaliwakutanisha washiriki mbalimbali kutoka
maeneo tofauti ndani na nje ya nchi kwa ajili ya kuonesha ubunifu, teknolojia
na fursa zilizopo katika sekta za uzalishaji.
Katika
maonesho hayo, Halmashauri ya Jiji la Dodoma ilitwaa nafasi ya kwanza katika
makundi ya Kilimo Ndani ya Uwanja, Mifugo Ndani ya Uwanja na Malisho Ndani ya
Uwanja kwa upande wa Kanda ya Kati.
Aidha,
jiji hilo lilipata nafasi ya pili katika kundi la Ufugaji Samaki katika
Maonesho ya Ndani ya Uwanja Kanda ya Kati na kutunukiwa tuzo maalum (trophy)
iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu
Hassan.
Mbali
na ushindi huo, Halmashauri ya Jiji la Dodoma pia ilishika nafasi ya pili
katika kundi la Jumla Mifugo Ndani ya Uwanja Kanda ya Kati, hivyo kukamilisha
jumla ya tuzo tano zilizotolewa katika maonesho hayo ya kitaifa.
Mafanikio
hayo yanaendelea kuthibitisha juhudi za Halmashauri ya Jiji la Dodoma katika
kuimarisha uzalishaji wa kilimo, kuboresha ufugaji na kuhamasisha matumizi ya
teknolojia bora kwa wakulima, wafugaji na wajasiriamali ili kuongeza tija na
kuchangia ukuaji wa uchumi.
Comments
Post a Comment