Katibu Mkuu Uchukuzi aipa tano TASAC kwa kuendelea kuwafikia wadau

Na. Immaculate Ruzika, DODOMA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Prof. Godius Kahyarara, leo ametembelea banda la Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) katika maonesho yanayoendelea kwenye viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma.

 



Akiwa katika banda hilo, Prof. Kahyarara alipatiwa maelezo kuhusu juhudi za TASAC katika kuhakikisha usalama, ulinzi na ubora wa huduma za usafiri wa majini kwa wananchi.

Akizungumza baada ya kutembelea banda hilo, Prof. Kahyarara aliipongeza TASAC kwa kushiriki maonesho hayo na kutumia jukwaa hilo kutoa elimu kwa wananchi kuhusu majukumu na huduma zake kwani elimu hiyo inasaidia kuongeza uelewa na kuimarisha ushirikiano kati ya taasisi na wananchi.

Maonesho hayo yenye kauli mbiu ya "Kuchochea Uwajibikaji Jumuishi kwa Huduma Endelevu" yalianza rasmi tarehe 16 na yanataria kufika tamati kesho tarehe 23 juni, 2026.

Comments