TANESCO wafanya usafi Soko la Machinga Dodoma

 Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kwa kushirikiana na maafisa kutoka Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Maafisa wa Kanda Namba Moja ya huduma pamoja na wafanyabiashara, wameungana kufanya usafi katika mitaro ya Soko la Wazi la Machinga, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kukabiliana na mvua kubwa zinazotarajiwa kunyesha.

 


Hatua hiyo inalenga kuhakikisha mitaro inakuwa safi na inapitisha maji kwa ufanisi, hivyo kupunguza athari zinazoweza kujitokeza wakati wa mvua, huku wafanyabiashara wakihimizwa kuendelea kutunza usafi wa mazingira katika maeneo yao kwa ustawi na usalama wa wote.





Comments

Popular Posts

Kata ya Matumbulu wanufaika na Mil. 114.7 Maadhimisho ya Samia Day

Samia Day 2026 yaibua vipaji vya michezo Kata ya Matumbulu