Kata ya Ipala yatekeleza agizo la usafi wa Mazingira
Na. Mwandishi wetu, IPALA Zoezi la uhamasishaji wa Usafi wa Mazingira katika Kanda Namba Saba limekua lenye mafanikio makubwa. Zoezi hilo limefanyika katika mitaa mitano iliyopo ndani ya Kata ya Ipala Mtaa wa Sokoine, Madukani, Azimio, Ukombozi na Mwinyi. Usafi wa Mazingira ulishilikisha wataalamu kutoka Kanda Namba Saba, wenyeviti wa mitaa, Diwani pamoja na wananchi waliojitoa kusafisha mitaa yote mitano kwa ushirikiano mkubwa kufuatia agiza la Mkuu wa Mkoa wa Dodoma la kusafisha Jiji la Dodoma kila siku. Akizungumza baada ya zoezi la Usafi wa Mazingira, DIwani wa Kata ya Ipala, Andrew Muhulo aliwapongeza wananchi kwa kujitokeza kwa wingi katika zoezi hilo la usafi wa Mazingira na kuwasihi wasiishie hapo tu maana zoezi la usafi ni maisha ya kila siku ya mtu mmoja mmoja. “Niwapongeze wananchi wote kwa kujitokeza kwenu kwa wingi mkuu wetu wa mkoa amesema zoezi la usafi ni la kila siku hivyo tudumishe usafi katika maeneo yote na viongozi kutoka ka...