Halmashauri ya Jiji la Dodoma yafanyia marekebisho Barabara ya kuingia Stendi ya Mnadani, Kizota
Na. Mwandishi wetu, KIZOTA
Halmashauri
ya Jiji la Dodoma inaendelea na zoezi la kufanya marekebisho ya barabara ya
kuingia katika Stendi ya Mnadani Kata ya Kizota, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa
maagizo yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule.
Hatua hiyo imekuja baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kuzungumza na wamiliki wa daladala na bajaji jana, ambapo alisisitiza umuhimu wa vyombo hivyo kuingia na kupaki ndani ya stendi badala ya kusimama na kupaki nje ya eneo la stendi, hali ambayo ni kinyume na utaratibu na sheria zilizowekwa.
Halmashauri
imeanza kuchukua hatua za haraka kuhakikisha mazingira ya kuingia na kutoka
katika Stendi ya Mnadani, Kata ya Kizota yanakuwa rafiki na salama kwa daladala,
bajaji, abiria na watumiaji wengine wa barabara.
Marekebisho
hayo yanatarajiwa kurahisisha utekelezaji wa maelekezo hayo na kuhakikisha
Stendi ya Mnadani Kata ya Kizota inatumika kwa utaratibu unaostahili, huku ikisaidia
kupunguza msongamano na usumbufu unaoweza kujitokeza nje ya stendi.
Halmashauri
ya Jiji la Dodoma inaendelea kusisitiza kwa wamiliki na waendesha vyombo vya
usafiri kuzingatia sheria, kanuni na maelekezo ya mamlaka husika katika
kuhakikisha usafiri wa umma unafanyika kwa usalama na utaratibu.
Comments
Post a Comment