Madiwani Dodoma wapongeza ukusanyaji mapato na utekelezaji Bajeti ya 2025/2026
Na. Tutindaga Nkwindi, DODOMA
Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Dodoma
limepokea taarifa ya utendaji kazi wa halmashauri kwa mwaka wa Fedha 2025/2026,
huku wajumbe wakipongeza juhudi za menejimenti katika ukusanyaji wa mapato na
utekelezaji wa bajeti.
Akiwasilisha taarifa hiyo, Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Vincent Odero alisema kuwa juhudi za ukusanyaji wa mapato zimeiwezesha halmashauri kutekeleza mipango na bajeti wake kwa ufanisi.
Kwa upande wake Mbunge wa Viti Maalum, Aisha Msantu
alisema kuwa menejimenti ya halmashauri imefanya kazi kubwa katika kukusanya
mapato na kuhakikisha yanatumika kutekeleza bajeti.
“Nawapongeza kwa kazi kubwa ya kukusanya mapato na
kuvuka lengo pia mmehakikisha yanatumika ipasavyo kutekeleza bajeti ya halmashauri”
alisema Msantu.
Nae Diwani wa Kata ya Ihumwa, Edward Magawa
ameipongeza menejimenti kwa utekelezaji wa bajeti na kusisitiza umuhimu wa
kusimamia vyanzo vya mapato, ikiwemo Soko la Job Ndugai na ‘Lorry Park’, ili
viweze kuleta tija na kuchangia maendeleo ya Jiji.
Baraza hilo limesisitiza umuhimu wa kuendelea kusimamia vyanzo vya mapato na kuhakikisha mapato yanayokusanywa yanatumika kwa malengo yaliyokusudiwa na kwa manufaa ya wananchi.
Comments
Post a Comment