Mwezi wa Maendeleo ya Jamii kujikita kutoa elimu ya Bima ya Afya Dodoma
Na. Mwandishi wetu, DODOMA
Halmashauri ya Jiji la Dodoma kuendelea kutoa elimu kwa
wananchi kuhusu umuhimu wa kuwa na bima ya afya, ikiwa ni sehemu ya shughuli
zinazofanyika katika Mwezi wa Maendeleo ya Jamii.
Akizungumza kuhusu elimu hiyo, Mratibu wa Mfuko wa Afya ya Jamii Iliyoboreshwa (iCHF) wa Jiji la Dodoma, Patrick Batimo, alisema kuwa wananchi wanapatiwa elimu kuhusu bima ya afya, ikiwemo Mfuko wa Afya ya Jamii Iliyoboreshwa (iCHF) pamoja na Bima ya Afya kwa Wote.
“Elimu hiyo inalenga kuwawezesha wananchi kuelewa
umuhimu wa bima ya afya na namna wanavyoweza kupata huduma za afya kupitia
mifumo hiyo”, alisema Batimo.
Aliongeza kuwa wananchi wanapaswa kutumia fursa ya
elimu inayotolewa ili kufahamu aina mbalimbali za bima ya afya, huduma
zinazopatikana pamoja na umuhimu wa kuwa na bima wakati wanapohitaji matibabu.
Aidha, utoaji wa elimu hiyo ni sehemu ya juhudi za
Halmashauri ya Jiji la Dodoma kuhakikisha wananchi wanafahamu huduma za bima ya
afya na umuhimu wa kujiunga na mifumo hiyo.
Hivyo, wananchi wametakiwa kushiriki katika shughuli za
Mwezi wa Maendeleo ya Jamii na kutumia fursa hiyo kupata elimu kuhusu bima ya
afya ili kuongeza uelewa na matumizi ya huduma hizo.
Comments
Post a Comment