Kata ya Ipala yatekeleza agizo la usafi wa Mazingira

Na. Mwandishi wetu, IPALA

 

Zoezi la uhamasishaji wa Usafi wa Mazingira katika Kanda Namba Saba limekua lenye mafanikio makubwa. Zoezi hilo limefanyika katika mitaa mitano iliyopo ndani ya Kata ya Ipala Mtaa wa Sokoine, Madukani, Azimio, Ukombozi na Mwinyi.

 


Usafi wa Mazingira ulishilikisha wataalamu kutoka Kanda Namba Saba, wenyeviti wa mitaa, Diwani pamoja na wananchi waliojitoa kusafisha mitaa yote mitano kwa ushirikiano mkubwa kufuatia agiza la Mkuu wa Mkoa wa Dodoma la kusafisha Jiji la Dodoma kila siku.

 

Akizungumza baada ya zoezi la Usafi wa Mazingira, DIwani wa Kata ya Ipala, Andrew Muhulo aliwapongeza wananchi kwa kujitokeza kwa wingi katika zoezi hilo la usafi wa Mazingira na kuwasihi wasiishie hapo tu maana zoezi la usafi ni maisha ya kila siku ya mtu mmoja mmoja.

 

“Niwapongeze wananchi wote kwa kujitokeza kwenu kwa wingi mkuu wetu wa mkoa amesema zoezi la usafi ni la kila siku hivyo tudumishe usafi katika maeneo yote na viongozi kutoka kanda watapita Kwenye maeneo yenu na kukagua namna usafi unavyofanyika” alisema Muhulo.

 


Kwa upande wao wataalamu kutoka Kanda Namba Saba wameahidi kuendelea kutoa elimu kwa wananchi katika kata zote na mitaa yote na kuhakikisha wananchi wanakua na uelewa juu ya maswala ya uhifadhi na utunzaji wa Mazingira.

 

Usafi wa Mazingira katika maeneno  yanayotuzunguka, majumbani, maeneo ya taasisi na sehemu zenye mkusanyiko wa biashara ni muhimu kufanyiwa usafi kwa kushirikiana wananchi wote, viongozi na wadau wa mbalimbali katika kuhifadhi Mazingira.

Comments

Popular Posts

Kata ya Miyuji Yaongeza Kasi ya Usimamizi Wa Usafi wa Mazingira

Kata za Nkuhungu na Kizota zajiandaa kukabiliana na mvua za El Nino

Zoezi la Kuua Mbwa Wanao Zurura Lafanyika Kata ya Msalato