Maadhimisho ya Mwezi wa Maendeleo ya Jamii kutilia mkazo usafi Dodoma

Na. Lulu Luvanda, DODOMA

Halmashauri ya Jiji la Dodoma imeandaa kampeni ya kuhamasisha wananchi kuhusu umuhimu wa usafi katika Maadhimisho ya Mwezi wa Maendeleo ya Jamii yanayofanyika jijini Dodoma Mwezi Septemba, 2026 kwa lengo la kuimarisha ushiriki wa jamii katika kutunza mazingira.

Akizungumza kuhusu maandalizi ya maadhimisho hayo Mkuu wa Divisheni ya Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma Charity Sichouna, alisema kuwa  wananchi watapewa elimu ya namna ya kuchangia katika utunzaji wa mazingira bora kupitia tabia sahihi za kila siku.

Alisema kuwa moja ya maeneo yatakayopewa kipaumbele ni usimamizi wa taka ngumu, ambapo wananchi wataelimishwa kuhusu namna ya kuzihifadhi na kuzitenganisha kulingana na aina zake kuanzia zinapozalishwa.

Kwa mujibu wa Sichona kutenganisha taka katika chanzo kutarahisisha ukusanyaji na uendeshaji wa taka, huku taka zinazoweza kutumika tena zikipata nafasi ya kurejelewa badala ya kuishia katika maeneo yasiyokusudiwa.

Alisema kuwa juhudi hizo zitaenda sambamba na kauli mbiu “Usafi ni Wajibu”, inayowataka wananchi kutambua nafasi yao katika kuhakikisha maeneo wanayoishi na kufanyia shughuli yanakuwa katika hali inayofaa.

Alisema kuwa maadhimisho hayo yatahusisha kliniki ya shughuli za maendeleo, ambapo wananchi watapata huduma na elimu kupitia madawati sita ya maendeleo, huku halmashauri ikishirikiana na wadau mbalimbali, ikiwemo UN-Habitat, kuhamasisha ushiriki wa jamii.

Aisha aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika shughuli za maadhimisho hayo na kutumia elimu watakayopewa kubadili tabia, ikiwemo kuhifadhi taka kwa usahihi na kushiriki katika shughuli zinazolenga kuboresha mazingira na maendeleo ya Jiji la Dodoma.

Comments

Popular Posts

Kata ya Miyuji Yaongeza Kasi ya Usimamizi Wa Usafi wa Mazingira

Kata za Nkuhungu na Kizota zajiandaa kukabiliana na mvua za El Nino

Mwenyekiti Mtaa wa Karume, Kata ya Mnadani ahamasisha usafi