Posts

Mikopo ya Makundi Maalum kurejeshwa Julai, 2024

Image
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Miko ana Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kurejesha utoaji wa mikopo kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu utakaoanza Julai, 2024. Akiwasilisha bungeni utekelezaji wa bajeti ya Mwaka 2023/24 na makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi hiyo kwa Mwaka 2024/25, Mchengerwa mikopo hiyo itaanza kwa utaratibu wa kutumia benki kwa halmashauri 10 za majaribio ambazo ni Dar  es Salaam, Dodoma, Kigoma Ujiji na Songea, Miji ya Newala na Mbulu, Wilaya za Siha, Nkasi, Itilima na Bumbuli. Aidha, alisema halmashauri 174 zilizobaki zitatumia utaratibu ulioboreshwa ili kuondoa mapungufu yaliyosababisha changamoto za awali kwa kufanya mambo yafuatayo; uanzishwaji wa kitengo cha usimamizi wa mikopo ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu katika Ofisi ya Rais – TAMISEMI, na uanzishwaji wa kamati za usimamizi wa mikopo katika ngazi za ofisi za wakuu wa mikoa, halmashauri na kata. “M...

Vipaumbele 13 vya mageuzi elimu msingi na sekondari 2024/2025

Image
OFISI ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa mwaka 2024/25 imepanga kutumia shilingi trilioni 1.02 ili kutekeleza vipaumbele 13 kwenye sekta ya elimu vinavyolenga kusimamia na kuendesha elimu msingi na Sekondari. Akiwasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka huo, Waziri wa Nchi, TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa alisema fedha hizo zitajenga  vyumba vya madarasa 6,357, matundu ya vyoo 1,482, umaliziaji wa mabwalo 362 kati ya mabwalo hayo 15 ni msingi na 347 ni ya sekondari na umaliziaji mabweni 36 kwenye shule za awali na msingi. Pia alisema shule mpya 184, nyumba za walimu 184 na mabweni 186 katika shule za sekondari yatajengwa, sambamba na ununuzi wa vifaa vya TEHAMA kwenye shule za awali tatu, msingi 400 na shule za sekondari 500, ununuzi wa kemikali za maabara katika shule mpya 234. Mchengerwa alisema fedha hizo zitatumika katika utoaji wa ruzuku ya elimu bila ada kwa shule za msingi 17,986 na sekondari 4,894; ununuzi na usambazaji wa vita...

Watanzania watakiwa kupambana na rushwa na dawa za kulevya

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA WATANZANIA wametakiwa kushikamana na kupambana na rushwa, dawa za kulevya na uvunjifu wa haki za binadamu ili kujenga jamii iliyo bora. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora, George Simbachawene Kauli hiyo ilitolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora, George Simbachawene alipokuwa akifungua mashindano ya mdahalo kwa shule za msingi, sekondari, vyuo vya kati na vyuo vikuu kuhusu madhara ya rushwa, matumizi ya dawa za kulevya, haki za binadamu na utawala bora katika ukumbi wa St. Gaspar Kisasa jijini Dodoma. Waziri Simbachawene alisema “baada ya watu kuwa wanashiba, elimu wanatapa kila kitu kinaenda vizuri, wanatazama televisheni wamepata ‘exposure’ mambo ni mazuri wameibuka maadui wengine. Maadui hao ni rushwa, dawa za kulevya na uvunjifu wa maadili na haki za binadamu, hao maadui watatu ni maadui wabaya sana, ni wajibu wa kila mmoja tushirikiane kupambana na maadui hao wa...

Shilingi Bilioni 1.5 kujenga Hospitali ya Wilaya Dodoma

Image
  Na. Dennis Gondwe, DODOMA SERIKALI imetoa shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Dodoma katika jitihada za kusogeza huduma bora za afya karibu zaidi na wananchi. Moja ya majengo ya Hospitali ya Wilaya ya Dodoma Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dkt. Andrew Method alipokuwa akiongelea mafanikio ya serikali ya awamu ya sita kwa kipindi cha miaka mitatu kwa waandishi wa habari ofisini kwake jijini hapa. Dkt. Method alisema “tunapoongelea mafanikio ya serikali ya awamu ya sita kwa kipindi cha miaka mitatu, mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa fedha shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Dodoma. Na hiyo hospitali ya wilaya ipo kimkakati kabisa, inajengwa eneo la Kata ya Nala. Ni eneo ambalo linaweza kufikiwa na rufaa ya vituo vyote vya afya ambavyo vinapitiwa na barabara ya mzunguko ‘ring road’. Kwa hiyo utaona hii barabara ya mzunguko inae...

Jiji la Dodoma lajenga vituo 8 vya Afya miaka 3 ya SSH

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA Halmashauri ya Jiji la Dodoma imeshuhudia ongezeko kubwa la ujenzi wa vituo vya afya nane katika serikali ya awamu ya sita inayolenga kuongeza miundombinu na kusogeza huduma za afya karibu na wananchi. Mkuu wa Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dkt. Andrew Method akielezea mafanikio ya divisheni yake Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dkt. Andrew Method alipokuwa akiongelea mafanikio ya miaka mitatu ya serikali ya awamu ya sita kwa waandishi wa habari ofisini kwake jijini hapa. “Ndugu waandishi wa habari, katika kipindi hiki cha miaka mitatu ya uongozi wa serikali ya awamu ya sita tumeshuhudia ongezeko kubwa la ujenzi wa vituo vya afya katika Jiji la Dodoma, tumejenga vituo vya afya nane. Mpaka sasa vituo viwili vimekamilika. Kituo cha Afya Chang’ombe kimekamilika. Mnafahamu eneo la Chang’ombe lina wakazi wengi zaidi ya 40,000 lakini hawakuwa n...

Miundombinu chachu ongezeko uandikishaji wanafunzi Jiji la Dodoma

Image
  UBORESHAJI wa miundombinu ya elimu unaoendelea kufanywa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan umekuwa chachu ya ongezeko la uandikishwaji wa wanafunzi wa darasa la kwanza na awali Jiji la Dodoma kutoka asilimia 98 hadi 115 kwa mwaka 2024. Mkuu wa Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Mwl. Prisca Myalla Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Mwl. Prisca Myalla alipokuwa akiongelea mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita kwa miaka mitatu ofisini kwake. “Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi Jiji la Dodoma tunampongeza sana Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha miundombinu ya elimu na kutujengea shule mpya kupitia mradi wa BOOST na EP4R. Halmashauri ya Jiji la Dodoma imeweza kujengewa madarasa mapya na kuboreshewa miundombinu hali iliyopelekea wazazi na jamii kuona fursa ya kuwaleta watoto wao kupata elimu. Serikali imejitahidi sana kuhakiki...

Jiji la Dodoma lapata hati safi miaka mitatu mfululizo

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma inajivunia kupata hati safi kwa miaka mitatu mfululizo kutokana na ushirikiano uliopo baina ya wataalam na Baraza la Madiwani katika kusimamia na kudhibiti matumizi sahihi ya fedha. Mkuu wa Kitengo cha Uhasibu na Fedha Halmashauri ya Jiji la Dodoma, CPA. David Rubibira alipokuwa akiongelea mafanikio ya serikali ya awamu ya sita Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Kitengo cha Uhasibu na Fedha Halmashauri ya Jiji la Dodoma, CPA. David Rubibira alipokuwa akiongelea mafanikio ya serikali ya awamu ya sita kwa miaka mitatu ofisini kwake. CPA. Rubibira alisema “kwa bahati nzuri kwa kipindi cha uongozi wa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Halmashauri ya Jiji la Dodoma imekuwa ikipata hati safi kwa miaka mitatu mfululizo. Hati inaangalia maeneo yafuatayo. Ukaguzi wa hesabu zilizowasilishwa na ukaguzi wa vitabu vilivyofanya malipo, nyaraka, viambata vyote na mchakato wa ukusanyaji mapato kama ulizingatia sheria, kanuni na taratibu. Hivyo, h...

TEHAMA chachu ya ukusanyaji mapato Jiji la Dodoma

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA Matumzi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma yamerahisisha shughuli za kutoa huduma kwa wananchi na kuongeza ukusanyaji wa mapato yakiziba mianya ya upotevu wa mapato. Mkuu wa Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Joseph Fungo akifafanua jambo Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Joseph Fungo alipokuwa akiongelea mafanikio ya serikali ya awamu ya sita katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Fungo alisema “matumizi ya TEHAMA yamerahisisha sana shughuli za serikali za kutoa huduma kwa wakati na kwa urahisi kwa wananchi. Serikali ya awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan imeiwezesha Halmashauri ya Jiji la Dodoma upatikanaji wa fedha kwenye ujenzi na uboreshaji wa mifumo ya TEHAMA ikiwemo mafunzo ya kuwajengea uwezo wataalam ili wawe na uelewa wa kutosha ...

Serikali yaboresha mazingira ya uwekezaji Jiji la DOdoma

Image
  Na. Dennis Gondwe, DODOMA Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan imetengeneza mazingira mazuri ya uwekezaji na kuwavutia wenye viwanda kuwekeza Halmashauri ya Jiji la Dodoma na kukuza uchumi. Kaimu Mkuu wa Divisheni ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Abeid Msangi Kauli hiyo ilitolewa na Kaimu Mkuu wa Divisheni ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Abeid Msangi alipokuwa akiongelea mafanikio ya serikali ya awamu ya sita kwa kipindi cha miaka mitatu ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Msangi alisema kuwa kwa mazingira mazuri ya uwekezaji yanayofanywa na serikali ya awamu ya sita, Halmashauri ya Jiji la Dodoma itaendelea kunufaika na uchumi wake kuanza kutegemea viwanda. “Katika kwenda sambamba na ongezeko la uwekezaji katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, tumejitika kufuata maelekezo ya Mpango Kabamba wa Jiji la Dodoma. Mpango huo umepanga m...

Shule ya Sekondari Michese kuwapunguzia umbali wanafunzi

Image