TEHAMA chachu ya ukusanyaji mapato Jiji la Dodoma
Na. Dennis Gondwe, DODOMA
Matumzi
ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma
yamerahisisha shughuli za kutoa huduma kwa wananchi na kuongeza ukusanyaji wa
mapato yakiziba mianya ya upotevu wa mapato.
Mkuu wa Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Joseph Fungo akifafanua jambo
Kauli
hiyo ilitolewa na Mkuu wa Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wa Halmashauri
ya Jiji la Dodoma, Joseph Fungo alipokuwa akiongelea mafanikio ya serikali ya
awamu ya sita katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
Fungo
alisema “matumizi ya TEHAMA yamerahisisha sana shughuli za serikali za kutoa
huduma kwa wakati na kwa urahisi kwa wananchi. Serikali ya awamu ya Sita
chini ya uongozi wa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan imeiwezesha Halmashauri ya
Jiji la Dodoma upatikanaji wa fedha kwenye ujenzi na uboreshaji wa mifumo ya TEHAMA
ikiwemo mafunzo ya kuwajengea uwezo wataalam ili wawe na uelewa wa kutosha
kuweza kufanyia kazi mifumo, miundombinu na vifaa vya TEHAMA kwa wakati”.
Akiongelea
mafanikio katika matumizi ya mifumo ya TEHAMA, alisema kuwa mifumo imeleta
mapinduzi makubwa. “Mfumo wa kukusanya mapato Tausi umesaidia katika ukusanyaji
wa mapato. Halmashauri ya Jiji vyanzo vyake vyote vya mapato vimeingizwa katika
mfumo wa Tausi na kukusanywa kieletroniki na hivyo, kuondoa mianya ya upotevu
fedha za Serikali. Kupitia TEHAMA tunaweza kufahamu mapato halisi ambayo
halmashauri inayapata na kuthibiti upotevu wa fedha na kuwafanya watumishi kuwa
makini katika maeneo yao ya ukusanyaji wa mapato. Kupitia mfumo wa Tausi
mwananchi anaweza kukata leseni ya biashara, vileo na leseni mbalimbali kwenye
mfumo akiwa nyumbani au sehemu yake ya biashara kwa kupitia simu yake ya
mkononi” alisema Fungo.
Akiongelea
mfumo wa huduma za Afya GOTHOMIS, alisema kuwa unatumika katika vituo vya Afya
na zahanati za serikali katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma. “Mfumo umesaidia
kuongeza usiri wa taarifa za mgonjwa, kuweka kumbukumbu sahihi za taarifa za
mgonjwa, kuongeza kiwango cha ukusanyaji mapato, kupunguza foleni na usumbufu
usio wa lazima. Kwa mfano, katika Kituo cha Afya Makole tangu tumeanza kutumia
mfumo wa GOTHOMIS kituo kilikuwa kinakusanya shilingi 12,000,000 kwa mwezi.
Baada ya kuanza kutumia mfumo mapato yalipanda hadi shilingi 36,000,000 kwa
mwezi. Hivyo, mfumo ulitusaidia sana kudhibiti upotevu mapato na kutoa huduma
kwa wagonjwa wengi zaidi kwa sababu ya urahisi wa kutumia mfumo huu” alisema
Fungo.
Wakati
huohuo, alisema kuwa halmashauri imejipambanua sana kwenye matumizi ya TEHAMA
kufikisha habari kwa wananchi. “Tunahakikisha sisi wenyewe tunakuwa mstari wa
mbele kutoa elimu kwa wananchi kupitia mitandao ya kijamii. Mfano tovuti ya Halmashauri
ya Jiji la Dodoma www.dodomacc.go.tz tumekuwa
tukiweka habari na taarifa mbalimbali za maendeleo na utekelezaji wa miradi ya
maendeleo iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa na mrejesho kutoka kwa
wananchi. Pia tunazo kurasa za mitandao ya kijamii kama Instagram, Facebook na
Youtube channel inayofahamika kama Dodoma City Tv” aliongeza.
Kitengo
cha TEHAMA kina jukumu la kusimamia mifumo, miundombinu, data na vifaa vya TEHAMA
katika uendeshaji wa shughuli za kila siku za Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
MWISHO
Comments
Post a Comment