Baraza la Madiwani Jiji la Dodoma lapitisha taarifa ya ufungaji hesabu 2025/2026
Na. Manase Malima, DODOMA
Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Dodoma
limeridhia na kuthibitisha taarifa ya ufungaji wa hesabu za halmashauri za hadi
kufikia tarehe 30 Juni, 2026 huku madiwani wakisisitiza umuhimu wa kuendeleza
uwazi na uwajibikaji katika uongozi na usimamizi wa fedha za umma.
Taarifa hiyo iliwasilishwa katika mkutano maalum wa Baraza la Madiwani uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, ambapo Mkuu wa kitengo cha Fedha na Uhasibu, CPA. David Rubibira aliwasilisha taarifa hiyo kwa ajili ya kuhakikiwa na kuthibitishwa na baraza.
CPA. Rubibira alisema kuwa taarifa za ufungaji wa
hesabu za halmashauri kwa tarehe 30 Juni, 2026 ikiwa ni sehemu ya utaratibu wa
kuwasilisha taarifa za kifedha kwa ajili ya kuhakikisha kuwa taarifa za halmashauri
zinaakisi hali halisi ya matumizi na usimamizi wa fedha.
Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Zuzu, Jenesta
Malingo alisema kuwa ameridhishwa na taarifa hiyo na anaamini kuwa uwazi katika
uwasilishaji wa taarifa za kifedha ni muhimu katika kuimarisha uongozi na
kujenga imani miongoni mwa wananchi.
Nae, Diwani wa Kata ya Mpunguzi, Isaya Chilongani alisema kuwa taarifa hiyo imewasilishwa kwa usahihi na alisisitiza umuhimu wa viongozi kuendelea kuwa wazi na kutoa taarifa kwa wakati, hatua ambayo alisema kuwa itasaidia kuimarisha uwajibikaji na uongozi bora katika halmashauri.
Comments
Post a Comment