Posts

Kliniki ya Kata ya Kikuyu Kaskazini kuwasogezea huduma wananchi mlangoni

Image
Na. Leah Mabalwe, DODOMA Wananchi wa Kata ya Kikuyu Kaskazini Jijini Dodoma wanatarajiwa kunufaika na huduma mbalimbali za serikali kupitia Kliniki ya Kata itakayoanzishwa wiki hii ikiwa ni hatua ya kusogeza huduma karibu na wananchi na kuwawezesha kupata huduma mbalimbali kwa urahisi. Hayo aliyazungumza Diwani wa Kata ya Kikuyu Kaskazini, Herry Beji nje ya ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Alisema kuwa Kliniki hiyo itafanyika kwa muda wa wiki moja katika Shule ya Msingi Kikuyu, ambapo idara na taasisi mbalimbali zitashiriki katika kutoa huduma kwa wananchi, miongoni mwa huduma zitakazopatikana ni huduma za ardhi. “Lengo letu ni kusogeza huduma karibu na wananchi ili wasipate usumbufu wa kwenda katika ofisi mbalimbali kutafuta huduma, ambapo wataalamu kutoka seksheni ya Ardhi ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma pamoja na Ofisi ya Kamishna wa Ardhi Mkoa wa Dodoma watakuwepo kusikiliza na kushughulikia changamoto mbalimbali za wananchi zinazohusu masuala ya Ardhi ...

Jiji la Dodoma lapongezwa kukusanya zaidi ya 100% mapato ya ndani Mwaka wa Fedha 2025/2026

Image
Na. Leah Mabalwe, DODOMA Halmashauri ya Jiji la Dodoma yapongezwa kwa namna inavyosimamia na kukusanya mapato, hatua inayochangia kwa kiasi kikubwa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika jiji hilo kufuatia ukusanyaji wa zaidi ya asilimia 100 kwa bajeti ya mwaka 2025/2026. Pongezi hizo zilitolewa na Mbunge wa Viti Maalum, Aisha Msantu mara baada ya kusomwa kwa taarifa ya tathmini ya mapato kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026, katika Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Dodoma lililofanyika katika ukumbi wa halmashauri hiyo. Alisema kuwa juhudi zinazoendelea kufanywa na halmashauri katika ukusanyaji na usimamizi wa mapato zinapaswa kupongezwa, huku akisisitiza umuhimu wa kuendelea kusimamia vyanzo vya mapato kwa ufanisi ili kuwezesha utekelezaji wa bajeti na mipango ya maendeleo ya jiji. “Nipende kuwapongeza halmashauri kwa namna ambavyo wanaendelea kukusanya na kusimamia mapato. Lakini pia katika utekelezaji wa bajeti ya jiji kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026, tunaona juhu...

Ufaulu elimu ya msingi wapanda Jiji la Dodoma hadi 94.3%

Image
Na. Mwandishi wetu, DODOMA   Ufaulu wa wanafunzi wa shule za msingi Jiji la Dodoma umeongezeka katika mitihani ya PSLE na SFNA, ukifikia asilimia 93.32 na 94.3 kwa Mwaka 2025, kutoka asilimia 89.15 na 88.9 Mwaka 2021.   Akizungumza wakati wa kuwasilisha taarifa ya utendaji kazi kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026, kwenye mkutano wa Mwaka cha Baraza la Madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa jiji hilo.    Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Vincent Odero alisema kuwa ongezeko hilo ni miongoni mwa mafanikio makubwa katika sekta ya elimu ya msingi, likionesha jitihada za halmashauri kuboresha elimu na kuongeza ufaulu wa wanafunzi.   “Ufaulu wa wanafunzi kwa miaka mitano kwa Darasa la Saba (PSLE) umeongezeka kutoka asilimia 89.15 kwa Mwaka 2021 hadi asilimia 93.32 Mwaka 2025. Aidha, ufaulu wa Darasa la Nne (SFNA) kwa miaka mitano umeongezeka kutoka asilimia 88.90 hadi asilimia 94.30, sawa na ongezeko la asilimia 5.4,” alisema Odero.   ...

Usafi wa mitaro na njia za maji Kusaidia kujikinga na mafuriko Dodoma Makulu

Image
Na. Amoni Sambulila, DODOMA   Wito umetolewa kwa wananchi kuhakikisha mitaro na njia za maji zinakuwa safi na wazi wakati wote, ili kuruhusu maji ya mvua kupita kwa urahisi na kuzuia maji kufurika na kuingia kwenye makazi ya wananchi.   Wito huo umetolewa na Kaimu Meneja wa Kanda Namba Nne, Evodius Canisto wakati wa zoezi la usafi wa mazingira lililofanyika katika kata hiyo ambapo aliwataka wananchi kufanya usafi katika maeneo yote yanayoweza kuathiriwa na maji ya mvua.   Evodius alisema kuwa mabadiliko ya tabianchi yanaweza kusababisha mvua kubwa na kwa nyakati tofauti hivyo wananchi wanapaswa kuchukua hatua mapema kwa kusafisha mitaro, kuondoa taka na vitu vingine vinavyoweza kuziba njia za maji.   Aliongeza kuwa usafi wa mazingira ni jukumu la kila mwananchi na haupaswi kufanyika wakati wa zoezi maalum pekee bali inapaswa kuwa sehemu ya maisha ya kila siku ili kulinda afya, usalama na mali za wananchi.   Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Shina en...

Mwenyekiti Mtaa wa Karume, Kata ya Mnadani ahamasisha usafi

Image
Na. Mwandishi wetu, MNADANI   Zoezi la usafi wa mazingira limehamasishwa katika Mtaa wa Karume, Kata ya Mnadani, kwa lengo la kuimarisha usafi na afya ya wananchi pamoja na kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira. Zoezi hilo pia limehusisha wataalam wa Kanda Namba Sita, ambao wamekuwa mstari wa mbele kutoa elimu na ushauri kwa wananchi kuhusu umuhimu wa usafi wa mazingira, utunzaji wa taka na namna ya kuzuia magonjwa yanayoweza kusababishwa na mazingira machafu.   Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Mwenyekiti wa Mtaa wa Karume, Waziri Matwiga amewataka wananchi kushiriki kikamilifu katika usafi wa mazingira na kujenga utamaduni wa kufanya usafi mara kwa mara.   “Usafi wa mazingira ni jukumu la kila mmoja wetu. Tunapaswa kushirikiana kuhakikisha mtaa wetu unakuwa safi na salama kwa afya ya wananchi,” amesema Matwiga.   Kwa upande wao, wataalam wa Kanda Namba Sita wameendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira, ikiwa ...

Kata ya Ihumwa yaanza usafi kutekeleza agizo la RC Dodoma

Na. Rahma Magona, DODOMA Kata ya Ihumwa katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma imeanza zoezi la usafi wa mazingira ikiwa ni hatua ya utekelezaji wa maagizo ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule ya kuhakikisha wananchi wanaimarisha usafi wa mazingira na kulinda afya zao.   Hatua hiyo imekuja baada ya viongozi wa Kata ya Ihumwa kuanza kuhamasisha wananchi kufanya usafi mtaa kwa mtaa kwa kushirikiana na maafisa afya kutoka Kanda Namba Mbili, huku ukaguzi wa vyoo katika kaya ukiwa miongoni mwa hatua zinazotekelezwa.   Akizungumza katika zoezi hilo, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Chang’ombe, Kata ya Ihumwa, Yoram Ndumizi alisema kuwa wamejipanga vizuri kuhakikisha wananchi wanashiriki katika usafi huku wakifanya ukaguzi wa vyoo baada ya kubaini baadhi ya kaya kutokuwa na vyoo, hali hiyo inaweza kuongeza hatari ya mlipuko wa magonjwa kutokana na uwezekano wa mvua nyingi za El Niño.   Ndumizi aliongeza kuwa kwa kushirikiana na maafisa afya, wanaendelea kut...

Wafanyabiashara Soko la Sabasaba wahimizwa usafi

Image
Na. Mohammed Ramadhani, DODOMA Wafanyabiashara katika Soko la Sabasaba jijini Dodoma wametakiwa kuendelea kufanya usafi wa mazingira kila siku badala ya kusubiri siku maalum ya usafi, hatua inayolenga kuweka mazingira ya biashara katika hali ya usalama na usafi. Akizungumza wakati wa zoezi la usafi katika Soko la Sabasaba, Afisa Mazingira wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Gwantwa Mbwile, alisema kuwa zoezi hilo limeanza tangu Jumatatu na kuendelea hadi Jumamosi, huku akiwataka wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla kufanya usafi kuwa sehemu ya maisha yao ya kila siku. Alisema kuwa kufanya usafi kila siku kunasaidia kupunguza muda na nguvu zinazotumika wakati wa kufanya usafi wa pamoja, kwani taka zinapokusanywa kwa muda mrefu huongezeka na kufanya zoezi kuwa gumu zaidi. “Wito wangu kwa wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla ni kujitahidi kuzoea kufanya usafi kila siku. Hii inarahisisha siku ambayo tunataka kufanya usafi maeneo yetu yanakuwa safi na hatuchukui muda mrefu. Si kusub...

Wananchi Dodoma Makulu wajitokeza kwa wingi zoezi la usafi wa Mazingira

Image
Na. Amoni Sambulila, DODOMA MAKULU Wananchi wa Kata ya Dodoma Makulu wamejitokeza kwa wingi kushiriki katika zoezi la usafi wa mazingira, ikiwa ni hatua ya kuhamasisha usafi na kuhakikisha mazingira yanakuwa safi na salama kwa jamii.   Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Msangalale Magharibi, Lucy Michael amewataka wananchi kuendelea kujitoa kwa wingi kufanya usafi na kuhakikisha unafanyika kila siku ili kuepuka magonjwa mbalimbali yanayoweza kusababishwa na uchafu wa mazingira. “Nawasihi wananchi wenzangu kujitokeza kwa wingi katika zoezi la usafi. Pia nasisitiza kuwa usafi wa mazingira ufanyike kila siku kwasababu utatuepusha na magonjwa mbalimbali yanayotokana na uchafu wa mazingira,” alisema Michael.   Kwa upande wake, Mwananchi Kalleb Wilson alisema kuwa wananchi wanapaswa kuendelea kushiriki katika zoezi la usafi wa mazingira na kuhakikisha maeneo yao yanakuwa safi wakati wote.   Nae, Afisa Biashara Kanda Namba Nne, Johari Fadhili...

Diwani Kata ya Miyuji azindua kampeni ya usafi wa Mazingira

Image
Na. Mwandishi wetu, MIYUJI   Diwani wa Kata ya Miyuji, Ringo Iringo, amezindua kampeni ya usafi wa mazingira kwa kushirikiana na wataalamu wa Kanda Namba Sita huku akiwataka wananchi kushiriki kikamilifu katika kuhakikisha mazingira yanakuwa safi na salama.   Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo, Iringo amesema kuwa usafi wa mazingira ni jukumu la kila mwananchi na kwamba juhudi za pamoja zinahitajika ili kukabiliana na changamoto ya uchafu katika maeneo ya makazi na maeneo ya wazi.   “Nawasihi wananchi wote tushirikiane katika kuhakikisha mazingira yetu yanakuwa safi. Usafi ni msingi wa afya bora na maendeleo ya jamii,” amesema Iringo.   Amesema kuwa kampeni hiyo inalenga kuhamasisha wananchi kuwa na utamaduni wa kufanya usafi mara kwa mara, kutunza maeneo yao na kuepuka kutupa taka hovyo.   Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Mtaa wa Miyuji Proper, Hawad Mbogela, amewataka wananchi kuunga mkono kampeni hiyo na kuhakikisha usafi unaendelea ...

Kata za Nkuhungu na Kizota zajiandaa kukabiliana na mvua za El Nino

Image
Na. Mwandishi wetu, DODOMA   Kanda Namba Tatu ya utoaji huduma katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma imefanya zoezi la usafi wa maeneo ya Kizota Relini na Mkonongo, Kata ya Nkuhungu, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kukabiliana na athari zinazoweza kusababishwa na mvua kubwa za El Niño.   Zoezi hilo lilihusisha ufunguaji na usafishaji wa mitaro, uondoaji wa taka pamoja na ukaguzi wa miundombinu ya kupitisha maji, hatua zinazolenga kupunguza hatari ya maji kujaa katika maeneo ya makazi na biashara.   Kaimu Meneja wa Kanda Namba Tatu, Vestina Manota aliwashukuru watumishi na wananchi kwa kushiriki katika zoezi hilo, akisema usafi wa mazingira ni muhimu katika maandalizi ya kukabiliana na athari za mvua za El Niño.   “Tunawahimiza wananchi kuendelea kufanya usafi kila siku na kuondoa taka kwenye mitaro ili kuhakikisha maji yanapata njia ya kupita kwa urahisi,” alisema Manota.   Diwani wa Kata ya Nkuhungu, Julius Ezekiel aliwataka wananchi kuchukua ta...