Mwenyekiti Mtaa wa Karume, Kata ya Mnadani ahamasisha usafi

Na. Mwandishi wetu, MNADANI

 

Zoezi la usafi wa mazingira limehamasishwa katika Mtaa wa Karume, Kata ya Mnadani, kwa lengo la kuimarisha usafi na afya ya wananchi pamoja na kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira.


Zoezi hilo pia limehusisha wataalam wa Kanda Namba Sita, ambao wamekuwa mstari wa mbele kutoa elimu na ushauri kwa wananchi kuhusu umuhimu wa usafi wa mazingira, utunzaji wa taka na namna ya kuzuia magonjwa yanayoweza kusababishwa na mazingira machafu.

 

Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Mwenyekiti wa Mtaa wa Karume, Waziri Matwiga amewataka wananchi kushiriki kikamilifu katika usafi wa mazingira na kujenga utamaduni wa kufanya usafi mara kwa mara.

 

“Usafi wa mazingira ni jukumu la kila mmoja wetu. Tunapaswa kushirikiana kuhakikisha mtaa wetu unakuwa safi na salama kwa afya ya wananchi,” amesema Matwiga.

 


Kwa upande wao, wataalam wa Kanda Namba Sita wameendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira, ikiwa ni pamoja na kuepuka kutupa taka hovyo, kuhakikisha taka zinakusanywa na kuwekwa katika maeneo yanayostahili, pamoja na kuzingatia usafi wa maeneo ya makazi na maeneo ya huduma za jamii.

 

Wataalam hao wamesisitiza kuwa usafi wa mazingira ni sehemu muhimu ya kinga dhidi ya magonjwa na unahitaji ushiriki wa wananchi, viongozi na wadau mbalimbali kwa pamoja.






Comments

Popular Posts

Kata ya Miyuji Yaongeza Kasi ya Usimamizi Wa Usafi wa Mazingira

Kata za Nkuhungu na Kizota zajiandaa kukabiliana na mvua za El Nino

Wafanyabiashara Soko la Miembeni Waazimia Kulinda Usafi