Wananchi Dodoma Makulu wajitokeza kwa wingi zoezi la usafi wa Mazingira

Na. Amoni Sambulila, DODOMA MAKULU

Wananchi wa Kata ya Dodoma Makulu wamejitokeza kwa wingi kushiriki katika zoezi la usafi wa mazingira, ikiwa ni hatua ya kuhamasisha usafi na kuhakikisha mazingira yanakuwa safi na salama kwa jamii.

 


Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Msangalale Magharibi, Lucy Michael amewataka wananchi kuendelea kujitoa kwa wingi kufanya usafi na kuhakikisha unafanyika kila siku ili kuepuka magonjwa mbalimbali yanayoweza kusababishwa na uchafu wa mazingira. “Nawasihi wananchi wenzangu kujitokeza kwa wingi katika zoezi la usafi. Pia nasisitiza kuwa usafi wa mazingira ufanyike kila siku kwasababu utatuepusha na magonjwa mbalimbali yanayotokana na uchafu wa mazingira,” alisema Michael.

 

Kwa upande wake, Mwananchi Kalleb Wilson alisema kuwa wananchi wanapaswa kuendelea kushiriki katika zoezi la usafi wa mazingira na kuhakikisha maeneo yao yanakuwa safi wakati wote.

 

Nae, Afisa Biashara Kanda Namba Nne, Johari Fadhili alisema kuwa upo umuhimu mkubwa kwa wananchi kuendelea kutunza mazingira yao kwa kufanya usafi mara kwa mara ikiwemo kuepuka magonjwa pamoja na faini zinazoweza kutolewa kutokana na kutokufanya usafi.

 

Zoezi la usafi limefanyika katika Kata ya Dodoma Makulu, huku wananchi wakihimizwa kuendeleza utamaduni wa kufanya usafi kila siku kwa ajili ya kulinda afya na mazingira ya jamii na kuliweka jiji safi.








Comments

Popular Posts

Kata ya Miyuji Yaongeza Kasi ya Usimamizi Wa Usafi wa Mazingira

Kata za Nkuhungu na Kizota zajiandaa kukabiliana na mvua za El Nino

Wafanyabiashara Soko la Miembeni Waazimia Kulinda Usafi