Kanda Namba Tatu yaimarisha ushirikiano na wamiliki wa vituo vya malezi ya watoto Dodoma

Na. Mwandishi wetu, DODOMA

Uongozi wa Kanda Namba Tatu umefanya kikao na wamiliki wa vituo vya malezi ya watoto (Daycare) vinavyopatikana ndani ya kanda hiyo kwa lengo la kuimarisha utoaji wa huduma za malezi na maendeleo ya watoto.


Akizungumza katika kikao hicho kilihofanyika katika Ofisi ua Kanda, Meneja wa Kanda Namba Tatu, CPA. Christina Changwala aliwataka wamiliki wa vituo hivyo kuhakikisha wanatoa malezi yanayozingatia maadili, mila na tamaduni za kitanzania ili kujenga kizazi chenye maadili mema na chenye mchango chanya katika maendeleo ya taifa.

 Aidha, aliwahimiza wamiliki wa vituo hivyo kuhakikisha wanakamilisha usajili wa vituo vyao ili vitambulike rasmi na viweze kuingizwa katika mifumo ya serikali ili kurahisisha usimamizi na utoaji wa huduma kwa mujibu wa sheria na taratibu.

Wamiliki hao pia walikumbushwa umuhimu wa kutimiza wajibu wa kulipa kodi na tozo mbalimbali zinazotozwa na Halmashauri ya Jiji la Dodoma pamoja na mamlaka nyingine husika, kwa wakati kwa kuwa mapato hayo ni nguzo muhimu katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo na utoaji wa huduma kwa wananchi.

Nae, Mmiliki wa Maximillian Daycare, Andrea Jeremia alisema kuwa wataendelea kushirikiana kwa karibu na uongozi wa Kanda Namba Tatu kwa kuhakikisha wanasimamia misingi imara ya malezi ya watoto, kulipa kodi na tozo za serikali kwa wakati, kushiriki katika shughuli za upandaji miti na kampeni nyingine za uhifadhi wa mazingira kwa lengo la kujenga mazingira bora kwa watoto na jamii kwa ujumla.






Comments

Popular Posts

Barabara za Mtaa wa Mbwanga yafunguliwa, Diwani Kerenge aitaja kuwa chachu ya maendeleo

BANDA YA JIJI LA DODOMA LATOA TEKNOLOJIA UFUGAJI SAMAKI NA KUKU PAMOJA