Barabara za Mtaa wa Mbwanga yafunguliwa, Diwani Kerenge aitaja kuwa chachu ya maendeleo

Na. Mwandishi wetu, Dodoma

Wakazi wa Mtaa wa Mbwanga katika Kata ya Mnadani wanatarajia kunufaika na usafiri rahisi, kuimarika kwa shughuli za biashara na kuongezeka kwa fursa za maendeleo kufuatia ufunguzi wa barabara za mtaa katika uboreshaji wa miundombinu kwa ajili ya maisha bora ya wananchi.


Akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi wa barabara hiyo, iliyofanyika katika moja ya barabara hizo, Diwani wa Kata ya Mnadani, Mugendi Kerenge alisema kuwa uboreshaji wa miundombinu ya barabara ni nguzo muhimu ya maendeleo kwa kuwa unarahisisha usafirishaji wa watu na bidhaa, kuchochea biashara na kuongeza upatikanaji wa huduma za kijamii.

“Kukamilika kwa barabara zaidi ya kilomita 14 zimefunguliwa  hii ni hatua muhimu katika safari ya maendeleo ya Kata ya Manadani. Itaondoa changamoto zilizokuwa zikiwakabili wananchi, hasa wakati wa mvua, na kufungua fursa zaidi za kiuchumi kwa wakazi wa Mbwanga na maeneo jirani. Natoa shukrani kwa Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma kwa kutuwezesha kufanikisha hili kwasababu haya ni baadhai ya mazimio katika Baraza la Madiwani mbapo iliadhimiwa kuwa barabara zote zifunguliwa na bahati nzuri mtaa wangu wa Mbwanga umekuwa wa kwanza kupata fursa hii” alisema Kerenge.

Aliwataka wananchi kuzitunza barabara hizo kwa kuepuka vitendo vinavyoweza kuziharibu, akisisitiza kuwa miundombinu ya umma ni mali ya wananchi wote na inapaswa kulindwa ili iendelee kutoa huduma kwa muda mrefu.


Aliongeza kwa kuwahimiza wakazi wa kata hiyo kuendelea kushirikiana na viongozi katika kutekeleza miradi ya maendeleo, akieleza kuwa kwa yeyote anayetaka kununua eneo kufuata taratibu ili kuepuka kuuziwa maeneo yaliyotengwa kwaajili ya barabara.

Kwa upande wake mkazi wa Mtaa wa Mbwanga, Jamira Rashid aliishukuru serikali kwa kufanikisha ufunguzi wa barabara hizo, akisema kuwa mradi huo utakuwa chachu ya maendeleo kwa wananchi.

“Barabara hizi ni ukombozi mkubwa kwa wananchi wetu kwa kuwa zitarahisisha usafiri, biashara na shughuli mbalimbali za maendeleo hata kama ikitokea dharura kama moto au mgonjwa basi gari litafika kiurahisi. Pia tunawashukuru wote waliohusika hadi kufikia hatua hii,” alisema Rashid.

Ufunguzi wa barabara katika Kata ya Mbwanga ni jambo ambalo litakwenda kuongeza kasi ya maendeleo kwasababu itarahisisha kupeleka na kufikia mindombinu ya shule, hospitali na maji.


 

Comments

Popular Posts

Kanda Namba Tatu yaimarisha ushirikiano na wamiliki wa vituo vya malezi ya watoto Dodoma

BANDA YA JIJI LA DODOMA LATOA TEKNOLOJIA UFUGAJI SAMAKI NA KUKU PAMOJA