Wananchi Dodoma wahimizwa kufanya usafi wa Mazingira kila siku
Na. Amoni Sambulila, MSALATO
Wananchi mkoani Dodoma wamehimizwa kufanya usafi wa mazingira kila siku na kuhakikisha
mazingira yanayowazunguka yanakuwa safi na salama kwa afya na ustawi wa jamii.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Usafi wa Mazingira mkoani Dodoma, uliofanyika katika eneo la Mnada wa Msalato, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyemule alisema kuwa kufanya usafi ni wajibu wa kila mwananchi na si jukumu la taasisi au mamlaka pekee.
Aliongeza Kwa kuwataka wananchi kushiriki kikamilifu
katika shughuli za usafi, kutunza maeneo yao na kuendelea kuzingatia usafi wa
mazingira katika maisha yao ya kila siku.
Kwa upande wake, mwananchi wa Msalato, Juma Ally alisema
kuwa ushiriki wa jamii ni muhimu katika kuhakikisha kampeni hiyo inakuwa na
matokeo chanya na kuleta mabadiliko katika maeneo mbalimbali.
Nae, mwananchi wa Msalato, Neema Ramadhani aliwahimiza
wananchi kufanya usafi kuwa sehemu ya maisha yao ya kila siku, ikiwemo kutunza
maeneo ya makazi na maeneo ya shughuli za kijamii.
Kampeni hiyo inalenga kuhamasisha jamii kuwa na
utamaduni endelevu wa usafi, pamoja na kuongeza uelewa kuhusu umuhimu wa
kutunza mazingira na kuhakikisha maeneo mbalimbali yanaendelea kuwa safi na
salama.
Comments
Post a Comment