DC Shekimweri agawa tisheti kwa wananchi waliojibu maswali ya usafi
Na. Mwandishi wetu, KIZOTA
Mkuu
wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri, ametoa zawadi za tisheti kwa
wananchi waliofanikiwa kujibu maswali mbalimbali kuhusu usafi na utunzaji wa
mazingira katika Mtaa wa Relini Kata ya Kizota.
Zawadi hizo zimetolewa ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha wananchi, hususan vijana, kuwa na uelewa kuhusu umuhimu wa usafi wa mazingira na kushiriki kikamilifu katika kampeni ya usafi jijini Dodoma yenye kaulimbiu isemayo “Dodoma Fahari Yetu, Usafi ni Wajibu Wetu.”
Comments
Post a Comment