CANADA YATOA BILIONI 240 KWENYE MFUKO WA AFYA WA PAMOJA
Na. Mwandishi wetu, DODOMA
Serikali ya Canada imetoa
kiasi cha shilingi
Bilioni 240 kwenye Mfuko wa Afya wa pamoja
(Health Basket Fund) ili kusaidia sekta ya Afya nchini.
![]() |
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu |
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu
alibainisha
hayo Julai
20, wakati wa mkutano wa utekelezaji wa shughuli za Mfuko wa Afya wa pamoja (Health
Busket Fund) na Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Canada jijini Dodoma.
“Tunaishuku sana Serikali ya Canada kupitia Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Canada, Mheshimiwa Harjit
Sajjani kwa
kusaidia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kiasi cha shilingi
Bilioni 240 kwa ajili ya kuboresha sekta ya afya”, alishukuru Waziri Ummy.
Aidha, alieleza kuwa kati ya kiasi hicho shilingi Bilioni 140 zinaingia serikalini kwa
ajili ya kuchangia Mfuko wa Afya wa Pamoja. Serikali ilishapokea
kiasi cha shilingi Bilioni 94 ambazo zimeelekezwa kwenye akaunti za ngazi ya
msingi ambazo ni zahanati na vituo vya afya nchini, alisema.
Vituo vya afya na zahanati watapanga vipaumbele vyao ikiwemo kununua dawa, uzazi salama, kulipia umeme, kulipia maji na wanatumia kufanya ukarabati mdogo pamoja na kununua vifaa tiba, aliongeza.
“Kwa ujumla mchango wa Serikali ya Canada kwa
Tanzania umeleta matokeo mazuri kwa huduma za afya Tanzania leo tunaongea wanawake karibu asilimia 90 wajawazito
wanajifungulia katika vituo vya kutoa huduma za afya kwa sababu ya mchango wa Canada”, alisema Waziri Ummy.
Pia aliongeza kuwa wamepunguza vifo vya watoto wachanga na wenye umri chini ya miaka
mitano kutoka vifo 67 katika kila vizazi hai 1,000 hadi vifo
43. “Lakini pia tumeweza kupunguza mimba za utotoni kutoka asilimia 27
hadi asilimia 22, tumepunguza udumavu kutoka asilimia 38 na sasa tunazungumzia
asilimia 31 na kwa watoto wetu wanapata chanjo”, alisema Waziri Ummy.
Kwa upande wake Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Canada Harjit Sajjani alisema kuwa wametangaza miradi mitano mipya ya Afya yenye thamani ya dola za Canada Milioni 128.5 ambapo dola za Canada Milioni 75 kwa mfuko wa ruzuku wa shughuli za Mfuko wa Afya wa pamoja (Health Sector Busket Fund) kwa Serikali ya Tanzania na nyongeza ya dola za Canada 500,000 kwa UNICEF kwa usaidizi wa kitaalam.
![]() |
Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Canada, Harjit Sajjani |
"Leo nina furaha pia kutangaza dola za Canada milioni
23 katika ufadhili wa Shirika la
CanGIVE kwa miradi miwili mipya kwa ushirikiano na UNICEF Tanzania na Shirika la
Afya Duniani, Tanzania miradi hii ya CanGive itasaidia juhudi za watanzania
kuchanja makundi yaliyopewa kipaumbele kwa njia ambayo itaimarisha huduma za Afya kwa
mapana zaidi”, alisema Sajjani.
MWISHO
Comments
Post a Comment