Wananchi Kata ya Msalato wapongezwa kujitokeza kwa wingi uzinduzi wa Kampeni ya Usafi wa Mazingira Dodoma

Na. Amoni Sambulila, MSALATO

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri amewapongeza na kuwashukuru wananchi kwa kujitokeza kwa wingi kushiriki katika uzinduzi wa Kampeni ya Usafi wa Mazingira mkoani Dodoma, uliofanyika katika eneo la Mnada wa Msalato, Halmashauri ya Jiji la Dodoma.



Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo, Alhaj Shekimweri alisema kuwa ushiriki wa wananchi unaonesha umuhimu wa jamii kushirikiana katika kutunza mazingira na kuhakikisha maeneo yanayowazunguka yanakuwa safi na salama.

Aliongeza kwa kuwataka wananchi kuendelea kufanya usafi katika maeneo yao na kushiriki kikamilifu katika shughuli za usafi ili kuimarisha afya na ustawi wa jamii.

Kwa upande wake, mwananchi wa Kata ya Msalato, Amani Merick alisema kuwa kampeni hiyo ni muhimu katika kuhamasisha jamii kuwa na utamaduni wa kutunza mazingira na kuzingatia usafi katika maeneo wanayoishi na kufanyia shughuli zao.

Nae, mkazi wa Dodoma, Hadija Yusuf aliwataka wananchi kuendeleza ushiriki wao katika shughuli za usafi na kuhakikisha mazingira yanabaki katika hali nzuri kwa manufaa ya jamii.

Usafi wa mazingira ni jukumu la jamii nzima, hivyo ushiriki wa kila mwananchi ni muhimu katika kuhakikisha maeneo ya makazi, biashara na maeneo ya umma yanakuwa safi na salama na pia  juhudi za kutunza mazingira zinahitaji ushiriki wa wananchi kwa kuendelea kufanya usafi.

Comments

Popular Posts

Jiji la Dodoma Biashara saa 24, usafi saa 24

Mvua za El Nino: DC Shekimweri awaasa wananchi wa Dodoma Kuchukua Tahadhari

Wananchi Dodoma wahimizwa kufanya usafi wa Mazingira kila siku