Vijana Dodoma na Iringa Kukutana Kupaza Sauti Dhidi ya Rushwa
Na. Muhamad Said, IRINGA
Wanafunzi
kutoka klabu za wapinga rushwa za shule za msingi na sekondari za mikoa ya
Dodoma na Iringa leo wanatarajiwa kukutana katika mdahalo maalumu wa mapambano
dhidi ya rushwa.
Mdahalo huo utafanyika katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Lugalo, mkoani Iringa, ukilenga kuwajengea wanafunzi uelewa, kuimarisha maadili na kuongeza ushiriki wa vijana katika mapambano dhidi ya rushwa ndani ya shule na jamii kwa ujumla.
Kupitia
mdahalo huo, wanafunzi wanatarajiwa kutoa hoja kuhusu madhara ya rushwa kwa
jamii na taifa pamoja na changamoto zinazoweza kujitokeza katika mapambano
dhidi ya vitendo hivyo. Aidha, mjadala unatarajiwa kutoa nafasi kwa vijana
kueleza namna wanavyoweza kuwa sehemu ya mabadiliko katika kujenga jamii
inayozingatia uadilifu.
Ushirikishwaji
wa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari unatarajiwa pia kuifanya shughuli
hiyo kuwa sehemu ya kuwaandaa vijana kuwa mabalozi wa maadili na mapambano
dhidi ya rushwa, kwa kuanza kujenga uelewa na msimamo wao tangu wakiwa katika
hatua za awali za elimu.
Mdahalo
huo unatarajiwa kuangazia pia umuhimu wa klabu za wapinga rushwa shuleni katika
kutoa elimu kwa wanafunzi, kuhamasisha uadilifu na kuwapa vijana nafasi ya
kujadili masuala yanayogusa maendeleo ya jamii.
Comments
Post a Comment