Diwani Kata ya Miyuji azindua kampeni ya usafi wa Mazingira
Na. Mwandishi wetu, MIYUJI Diwani wa Kata ya Miyuji, Ringo Iringo, amezindua kampeni ya usafi wa mazingira kwa kushirikiana na wataalamu wa Kanda Namba Sita huku akiwataka wananchi kushiriki kikamilifu katika kuhakikisha mazingira yanakuwa safi na salama. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo, Iringo amesema kuwa usafi wa mazingira ni jukumu la kila mwananchi na kwamba juhudi za pamoja zinahitajika ili kukabiliana na changamoto ya uchafu katika maeneo ya makazi na maeneo ya wazi. “Nawasihi wananchi wote tushirikiane katika kuhakikisha mazingira yetu yanakuwa safi. Usafi ni msingi wa afya bora na maendeleo ya jamii,” amesema Iringo. Amesema kuwa kampeni hiyo inalenga kuhamasisha wananchi kuwa na utamaduni wa kufanya usafi mara kwa mara, kutunza maeneo yao na kuepuka kutupa taka hovyo. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Mtaa wa Miyuji Proper, Hawad Mbogela, amewataka wananchi kuunga mkono kampeni hiyo na kuhakikisha usafi unaendelea ...