Kanda Namba Moja yaadhimisha Miaka 62 ya Muungano kwa kufanya Usafi

 

Viongozi wa Kanda Namba Moja, viongozi wa kata na mitaa pamoja na wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla, wameungana kushiriki zoezi la usafi katika Kata ya Uhuru kwa kusafisha mitaro ya maji ya mvua iliyopo kando ya barabara. Zoezi hilo limefanyika kwa lengo la kuimarisha usafi wa mazingira na kuhakikisha usalama wa afya za wananchi. Aidha, zoezi hilo lilifanyika ikiwa sehemu ya maandalizi ya kuelekea katika maadhimisho ya miaka 62 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, yenye kaulimbiu isemayo: "Miaka 62 ya Muungano: Amani na Mshikikamano ni Msingi wa Maendeleo Endelevu".








Kupitia zoezi hilo, wananchi walikumbushwa umuhimu wa kudumisha usafi wa mazingira kila siku, bila kusubiri usafi wa jumamosi ya mwisho wa mwezi au wakati wa maadhimisho ili kujenga jamii yenye afya bora na maendeleo endelevu.

 

Comments

Popular Posts

Juhudi na nidhamu yatakiwa kwa washiriki wa mafunzo ya Jeshi la Akiba Dodoma

Wanafunzi Dodoma watakiwa kutoa taarifa za ukatili wa kijinsia