Huduma ya Maji kuimarika Dodoma

Na. Dennis Gondwe, DODOMA

HALI ya upatikanaji wa huduma ya Maji safi na salama imeendelea kuimarika hadi kufikia lita 88.7 kwa siku sawa na asilimia 55 ya mahitaji yote.


Kauli ilitolewa na Katibu Tawala Wilaya ya Dodoma, Sakina Mbugi alipokuwa akisoma Risala ya Utii kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Wilaya ya Dodoma katika uwanja wa Shule ya Msingi Kizota jijini Dodoma.

Alisema kuwa hali ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama ni lita Mil. 88.7 kwa siku sawa na asilimia 55 ya mahitaji ya wakazi wote ambayo ni lita Mil. 159.9. DUWASA imeendelea kutekeleza miradi 38 ya shilingi bilioni 91. ambayo ikikamilika itaongeza upatikanaji wa Maji kwa zaidi ya asilimia 75 ya mahitaji ya siku.

MWISHO

 

Comments

Popular Posts

Wafanyabiashara Soko la Miembeni Waazimia Kulinda Usafi

Baraza la Madiwani Jiji la Dodoma lapitisha taarifa ya ufungaji hesabu 2025/2026

Wilaya ya Dodoma kuchanja watoto zaidi ya laki 2 chanjo ya Polio