Shilingi Bil. 2.1 zatolewa kujenga miundombinu Sekta ya Afya

Na. Dennis Gondwe, DODOMA

WILAYA ya Dodoma imepokea shilingi 2,145,756,727.12 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu na ununuzi wa samani na vifaa tiba katika jitihada za serikali kuboresha huduma za afya wilayani hapa.


Kauli hiyo ilitolewa na Katibu Tawala Wilaya ya Dodoma, Sakina Mbugi alipokuwa akisoma Risala ya Utii kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Wilaya ya Dodoma katika uwanja wa Shule ya Msingi Kizota jijini Dodoma.

Alisema kuwa katika kipindi cha Mwaka wa Fedha 2025/2026 wilaya ilipokea kiasi cha shilingi 2,145,756,727.12 kwa ajili ya sekta ya afya. “Kati ya fedha hizo shilingi 1,945,756,727.12 ni kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya afya na kiasi cha shilingi 200,000,000 ni kwa ajili ya ununuzi wa samani na vifaa tiba. Wilaya inakamilisha ujenzi wa Hospitali ya Jiji, Kituo cha Afya Zuzu, Chang’ombe, Msalato, Zahanati ya Kiwanja cha Ndege, Tambukareli na Jengo jumuishi Makole. Fedha hizi zimetoka serikali kuu na Halmashauri ya Jiji” alisema Mbugi.

Mwenge wa Uhuru Mwaka 2026 unaongozwa na kaulimbiu isemayo ‘Tanzania ni Yetu Sote, Tushikamane kwa pamoja Kuleta Maendeleo ’.

MWISHO

 

Comments

Popular Posts

Wilaya ya Dodoma yapata “clean sheet” Miradi ya Mwenge wa Uhuru 2026