Dodoma kupambana na VVU
Na. Dennis Gondwe, DODOMA
WILAYA ya Dodoma imeendelea kupambana na
maambukizi ya Virusi vya UKIMWI (VVU) ikiwa na maambukizi ya asilimia 2.7 kwa Mwaka 2025.
Kauli hiyo ilitolewa na Katibu Tawala Wilaya ya Dodoma, Sakina Mbugi alipokuwa akisoma Risala ya Utii kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Wilaya ya Dodoma katika uwanja wa Shule ya Msingi Kizota jijini Dodoma.
Alisema kuwa mapambano dhidi ya maambukizi ya
Virusi vya UKIMWI yanapewa uzito mkubwa. ”Mheshimiwa Rais, hali ya ushamiri wa maambukizi ya VVU wilayani kwa mwaka 2025 ni
asilimia 2.7. Aidha, chini ya Kaulimbiu inayosema “Imarisha mwitikio; Tokomeza UKIMWI”, kwa kipindi cha
Januari, 2025 hadi Desemba, 2025 jumla ya watu 89,562 (Me 34,806 Ke 54,756) walijitokeza kupima maambukizi ya Virusi vya UKIMWI
kwa hiari, kati yao watu 2,432 walikutwa na maambukizi na kuunganishwa na
huduma za tiba na matunzo kwa WAVIU.
Hata hivyo, katika kuhakikisha tunafikia lengo la kitaifa la 95-95-95 ifikapo mwaka 2030, hadi kufikia Aprili, 2026
asilimia 96.3 ya
watu wanaoishi na maambukizi ya VVU walitambua hali zao na kati yao asilimia 97.7 wanatumia dawa za kufubaza virusi
vya UKIMWI na asilimia 95.6
wamefanikiwa kufubaza chini ya nakala 1,000.
Aidha, elimu
imeendelea kutolewa kwa jamii kwa njia ya redio na warsha ili kudhibiti
maambukizi mapya” alisema Mbugi.
Mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI
yanaongozwa na kaulimbiu inayosema “Imarisha
mwitikio; Tokomeza UKIMWI”.
MWISHO
Comments
Post a Comment