Jiji la Dodoma lachangia Mil. 70 Mwenge wa Uhuru 2026

Na. Dennis Gondwe, DODOMA

HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imechangia shilingi 70,000,000 kufanikisha Mbio za Mwenge wa Uhuru katika Wilaya ya Dodoma Mwaka 2026 zilizoongozwa na kaulimbiu isemayo ‘Tanzania ni Yetu Sote, Tushikamane kwa pamoja Kuleta Maendeleo’.



Kauli hiyo ilitolewa na Katibu Tawala Wilaya ya Dodoma, Sakina Mbugi alipokuwa akisoma Risala ya Utii kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Wilaya ya Dodoma katika uwanja wa Shule ya Msingi Kizota jijini Dodoma.

Akiongelea michango ya Mbio za Mwenge wa Uhuru 2026, alisema kuwa ulichangiwa na sekta ya umma na sekta binafsi. ”Mheshimiwa Rais, Mbio za Mwenge wa Uhuru Mwaka 2026 zimechangiwa michango yenye jumla ya shilingi 100,944,500. Wananchi wamechangia shilingi 24,044,500, Halmashauri ya Jiji la Dodoma shilingi 70,000,000 na sekta binafsi pamoja na Mashirika ya Umma shilingi 6,900,000. Kati ya fedha hizo shilingi 5,460,000 zimerejeshwa kuchangia ununuzi wa viti 40 na meza 40 vitakavyotumika katika shule za sekondari zenye uhitaji.

Mwenge wa Uhuru Mwaka 2026 unaongozwa na kaulimbiu isemayo ‘Tanzania ni Yetu Sote, Tushikamane kwa pamoja Kuleta Maendeleo’.

MWISHO

 

Comments

Popular Posts

Wilaya ya Dodoma yapata “clean sheet” Miradi ya Mwenge wa Uhuru 2026