Dodoma Jiji FC yawaalika mashabiki kujitokeza kwa wingi dhidi ya Namungo

Na. Amoni Sambulila, DODOMA

Timu ya Dodoma Jiji FC imewaalika mashabiki wa klabu hiyo kujitokeza kwa wingi katika mchezo dhidi ya Timu ya Namungo utakaofanyika leo Ijumaa majira ya saa moja usiku katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.



Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuelekea mchezo huo, Msemaji wa Timu ya Dodoma Jiji FC, Moses Mpunga amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanjani na kuendelea kuipa timu yao sapoti katika mchezo huo.

“Uwepo wa mashabiki kwa wingi uwanjani ni muhimu kwa timu yetu, kwasababu sapoti yao inaweza kuongeza morali na kuipa nguvu Timu ya Dodoma Jiji FC katika kipindi chote cha mchezo” amesema Mpunga.

Aliongeza kuwa wanatambua mchango wa mashabiki katika kuisapoti timu na hivyo kuwaomba waendelee kujitokeza katika michezo ya timu hiyo, hasa katika mchezo huo dhidi ya Namungo.

MWISHO

Comments

Popular Posts

Wafanyabiashara Soko la Miembeni Waazimia Kulinda Usafi

Kata ya Miyuji Yaongeza Kasi ya Usimamizi Wa Usafi wa Mazingira

Vijana Dodoma na Iringa Kukutana Kupaza Sauti Dhidi ya Rushwa