Ziara ya DC kukagua ujenzi wa Barabara Dodoma

 

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mhe. Alhaj Jabir Shekimweri, ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara tatu zinazotekelezwa na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma.


     Barabara Nzuguni – kwa Masista (KM 0.5) kwa kiwango cha lami, pamoja na Barabara ya Nzuguni – Makaburini (KM1.5) kwa kiwango cha changarawe, ikiwa na gharama ya shilingi milioni 694.1 fedha kutoka Road Fund Development.

     Mradi wa uboreshaji wa Barabara ya Mwangaza (KM1.1) kwa kiwango cha lami, kwa gharama ya shilingi Bilioni 1.6.

     Mradi wa uboreshaji wa Barabara ya Mwangaza – Mwambosa (KM 0.7) kwa kiwango cha lami, gharama ya mradi ni shilingi milioni 880.1.





Comments

Popular Posts

Vijana watakiwa kujiendeleza nje ya mfumo rasmi

NGOs zatakiwa kuzingatia uwazi na uwajibikaji Dodoma