Miundombinu ya elimu kuing’arisha Msembeta S/M
Na. Jesca Kipingu, DODOMA
Mradi wa umaliziaji wa ujenzi wa matundu 13 ya vyoo katika
Shule ya Msingi Msembeta, umefikia asilimia 90 ya utekelezaji, ambapo kazi
mbalimbali za ujenzi na umaliziaji wa miundombinu hiyo zinaendelea kwa kasi
kuelekea kukamilika kwake.
Mradi huo unatekelezwa kwa gharama ya shilingi 38,905,912.75,
fedha zinazotokana na mapato ya ndani ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
Sambamba na hilo, halmashauri imefanikiwa kukamilisha
kwa asilimia 100 mradi wa umaliziaji wa nyumba moja ya mwalimu katika Shule ya
Msingi Msembeta. Mradi huo umegharimu jumla ya shilingi 40,100,000, fedha
ambazo pia zimetolewa kupitia mapato ya ndani ya halmashauri.
Kukamilika kwa miradi hii kunatarajiwa kuleta nafuu
kwa walimu na wanafunzi, huku kukiwa na ongezeko la mazingira bora ya
ufundishaji na ujifunzaji. Uwekezaji huo unaendelea kuonesha dhamira ya
Halmashauri ya Jiji la Dodoma katika kuimarisha sekta ya elimu kwa kutambua
kuwa miundombinu bora ni msingi muhimu wa utoaji wa elimu yenye ubora.
Halmashauri ya Jiji la Dodoma inaendelea kuelekeza miradi
yenye manufaa kwa wananchi kupitia mapato ya ndani, kwa lengo la kuhakikisha
maendeleo yanafika katika maeneo mbalimbali na kuboresha huduma muhimu za
kijamii.
#Mapato ya Ndani kwa Maendeleo ya Dodoma Jiji.
#DodomaJiji #MapatoYaNdani #Elimu #Msembeta
#MiradiYaMaendeleo #MiundombinuYaElimu
Comments
Post a Comment