Posts

Polisi yaokoa fedha, yaongeza ujenzi wa jengo la ghorofa tatu mradi wa makazi Dodoma

Image
Na. Mwandishi wetu, DODOMA Jeshi la Polisi Wilaya ya Dodoma limepongezwa kwa kufanikiwa kuokoa fedha katika utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa majengo ya makazi ya askari wa vyeo vya ‘rank and file’ hatua iliyowezesha kuongeza jengo moja la ghorofa tatu licha ya mradi awali kulenga kujenga majengo manane.   Akizungumza wakati wa kukagua maendeleo ya mradi huo eneo la Kutuliza Ghasia Jiji la Dodoma, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri alikipongeza Kikosi Kazi cha Ujenzi cha Jeshi la Polisi kwa kutumia rasilimali zilizopo kwa ufanisi na kuwezesha kuokoa fedha za umma.   Alisema kuwa hatua hiyo ni mfano wa namna taasisi za serikali, hususan vyombo vya ulinzi na usalama, zinavyoweza kutanguliza uzalendo na matumizi bora ya fedha za umma katika kutekeleza miradi ya maendeleo.   “Kwa hili tunawapongeza kwa dhati. ‘Mme-demonstrate’ kama vyombo vya ulinzi na usalama mkipewa majukumu haya ya nchi, mnatanguliza mbele uzalendo na kuokoa fedha za umma. Hili ni...

Familia 96 kunufaika na mradi wa makazi ya Askari Polisi Dodoma

Image
Na. Mwandishi wetu, DODOMA Jumla ya familia 96 za askari wa vyeo ‘Rank and File’ eneo la kutuliza ghasia wilayani Dodoma zinatarajiwa kunufaika na mradi wa ujenzi wa majengo manane ya ghorofa tatu, unaolenga kuboresha makazi yao kwa kuwapatia nyumba bora, salama na zenye viwango vya kisasa.   Mradi huo umefikia asilimia 73 ya utekelezaji, ambapo kila jengo katika mradi huo limepangwa kuhudumia familia 12, huku majengo matano kati ya manane yakiwa yamekamilika na matatu yakiwa katika hatua mbalimbali za ukamilishaji. Akizungumza wakati wa kutembelea mradi huo, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri alilipongeza Jeshi la Polisi kwa hatua waliyofikia, akibainisha kuwa ujenzi huo ni sehemu muhimu ya maboresho ya mazingira ya makazi ya askari. “Tunawapongeza kwa hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa mradi huu, na tunawapongeza zaidi kwa kuhakikisha kwamba majengo matano yameshakamilika, huku majengo matatu yakiwa katika hatua mbalimbali za ukamilishaji. Kwa hatua hii...

Kituo Kikuu cha Polisi Dodoma kuunganishwa na mifumo ya TEHAMA

Image
Na. Mwandishi wetu, DODOMA Kituo Kikuu cha Polisi Daraja A kinachojengwa Wilaya ya Dodoma kinatarajiwa kufungwa mfumo wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), ikiwamo CCTV na chumba maalumu cha udhibiti (control room), kwa lengo la kuimarisha ufuatiliaji wa usalama na udhibiti wa uhalifu mara baada ya kukamilika kwa ujenzi.   Hatua hiyo ilielezwa wakati wa ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho pamoja na majengo manane ya ghorofa tatu ya makazi ya askari wa vyeo vya ‘Rank & File’ katika eneo la kutuliza ghasia, Jiji la Dodoma.   Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri, alisisitiza umuhimu wa kuwepo kwa chumba maalumu cha ufuatiliaji na udhibiti wa mfumo huo, chenye mazingira rafiki ya kazi na vifaa vya kisasa. Alisema kuwa matumizi ya CCTV yatasaidia kufuatilia hali ya usalama, kuimarisha usalama barabarani, kudhibiti msongamano wa magari, kupanga doria za kimkakati na kurahisisha upatikanaji wa ushahidi w...

Ujenzi wa Kituo cha Polisi Dodoma wafikia 61%

Image
Na. Mwandishi wetu, DODOMA Ujenzi wa Kituo cha Polisi Daraja A katika Wilaya ya Dodoma umefikia asilimia 61, kwa lengo la kukabiliana na changamoto ya ufinyu wa nafasi na uchakavu wa miundombinu ya kituo cha zamani, ambayo ilikuwa ikikwamisha utoaji wa huduma bora kwa wateja.   Mradi huo unatekelezwa kwa fedha za ndani kupitia Mfuko wa Tuzo na Tozo, ambapo shilingi milioni 900 zilikuwa zimepokelewa, kati ya fedha hizo shilingi 825,916,511.27 zimetumika katika ujenzi huo.   Akielezea kuhusu maendeleo ya mradi huo, Mhandisi wa Polisi, ASP Gaston Nombo alisema kuwa kukamilika kwa kituo hicho kikubwa na cha kisasa kutawezesha kuwepo kwa mazingira salama na rafiki kwa watumiaji wa ndani na nje ya Jeshi la Polisi, jambo litakaloongeza ustawi na tija kwa watendaji pamoja na kuimarisha utoaji wa huduma bora kwa wananchi.   “Tumepata fedha kutoka serikali kuu, tumeambiwa tutaletewa fedha kama shilingi bilioni moja. Mradi huu unatekelezwa kwa mfumo wa nguvu kazi, ambapo...

Dodoma Jiji FC yajiwinda dhidi ya Namungo dimba la Jamhuri

Image
Na. Amoni Sambulila, DODOMA Timu ya Dodoma Jiji FC imeendelea na maandalizi kuelekea mchezo wa raundi ya sita wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara dhidi ya Timu ya Namungo FC, utakaochezwa leo Ijumaa majira ya saa moja usiku katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma. Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari kuelekea mchezo huo, Kocha Mkuu wa Timu ya Dodoma Jiji FC, Vicent Mashami alisema kuwa timu yake ipo katika hali nzuri baada ya kupata ushindi katika michezo miwili iliyopita, huku akisisitiza umuhimu wa kuendeleza mwenendo huo wa ushindi. “Timu ipo vizuri, ambapo mechi mbili zilizopita tulipata ushindi na hivyo tunahitaji kuwa na mwendelezo wa ushindi. Pia Namungo ni timu yenye ubora na ushindani, licha ya kupoteza mechi tatu zilizopita, hivyo tunatambua mchezo huu hautakuwa rahisi,” alisema Mashami. Kwa upande wake, mchezaji Mwanakibuta David, alisema kuwa wachezaji wako tayari kupambana katika mchezo huo na kuhakikisha wanaendelea kupata matokeo mazuri. “Tunajua mchezo ...

Dodoma Jiji FC yawaalika mashabiki kujitokeza kwa wingi dhidi ya Namungo

Image
Na. Amoni Sambulila, DODOMA Timu ya Dodoma Jiji FC imewaalika mashabiki wa klabu hiyo kujitokeza kwa wingi katika mchezo dhidi ya Timu ya Namungo utakaofanyika leo Ijumaa majira ya saa moja usiku katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma. Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuelekea mchezo huo, Msemaji wa Timu ya Dodoma Jiji FC, Moses Mpunga amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanjani na kuendelea kuipa timu yao sapoti katika mchezo huo. “Uwepo wa mashabiki kwa wingi uwanjani ni muhimu kwa timu yetu, kwasababu sapoti yao inaweza kuongeza morali na kuipa nguvu Timu ya Dodoma Jiji FC katika kipindi chote cha mchezo” amesema Mpunga. Aliongeza kuwa wanatambua mchango wa mashabiki katika kuisapoti timu na hivyo kuwaomba waendelee kujitokeza katika michezo ya timu hiyo, hasa katika mchezo huo dhidi ya Namungo. MWISHO

Heri ya Mtihani Darasa la Saba Wilaya ya Dodoma

Image
 

Faini 300,000 wachafuzi wa Mazindira Dodoma

Image
 

DC Shekimweri awatakia Heri ya Mtihani wanafunzi wa Darasa la Saba Dodoma

Image
 

Meya Chaula awatakia Heri Darasa la Saba Dodoma

Image