Elimu ya MEMKWA, Fursa ya Pili

Na. Muhamad Kulele, DODOMA

 

Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma amesema kuwa elimu ya MEMKWA imeendelea kuwa daraja muhimu kwa wale ambao hawakupata nafasi ya kuendelea na elimu katika mfumo wa kawaida.



Mwakilishi huyo ambae ni Afisa Elimu wa Mkoa wa Dodoma, Kiduma Mageni alisema hayo alipomuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma katika kilele cha Juma la Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi, kilichofanyika katika viwanja vya Nyerere Square, jijini Dodoma.

Alisema kuwa elimu ya MEMKWA imeendelea kuwa daraja muhimu kwa wale ambao hawakupata nafasi ya kuendelea na elimu katika mfumo wa kawaida. Alisema kuwa yeye binafsi ameshuhudia jitihada za MEMKWA katika kuwapatia wananchi fursa ya kusoma, kuandika, kuhesabu na kujenga ujuzi wa maendeleo.

Aidha, alisisitiza kuwa elimu haina umri, fursa ya kujifunza haipaswi kufungwa na wakati.




 

Comments

Popular Posts

Vijana watakiwa kujiendeleza nje ya mfumo rasmi

NGOs zatakiwa kuzingatia uwazi na uwajibikaji Dodoma

Ziara ya DC kukagua ujenzi wa Barabara Dodoma